Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ujasiriamali.. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ujasiriamali.. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 1 Novemba 2017

Akili yako ndio mtaji wako!!!

"Ni kipi kinachemka ndani yako"!???
Mpendwa msomaji,
Ni muhimu kufahamu kila binadamu anachokitu ndani mwake chenye msukumo mkubwa kukifanya na wakati mwingine kinakupa majibu kuwa hii ndiyo dili itakayo nifanya nifanikiwe. Sauti hiyo kamwe usipuuze ikiwa tuu unaliona ni jambo jema!!!.
Katika hali ya asili ya mwanadamu ya kawaida utaona iko sauti nyingine inayokuja ikiwa na nguvu kuliko Ile ya kwanza na itakuletea vikwazo vingi sana! Nasema ipuuze sauti hiyo, kwani haikutakii mema bali ni sauti ya maadui wa maono yako!
Kadhalika usitegemee watu utakao waingiza kukusaidia kukufikisha unakotaka kwenda kuwa watakufikisha sawasawa na utakavyo ikiwa hauna usimamizi mzuri. Kwakuwa wewe ndiye uliyebeba ramani ya biashara au shughuli zako, hivyo usitegemee wasaidizi wako wanaweza kukufikisha kule unakotaka kufikia ikiwa hauna uangalizi wa karibu. Na pia hujaweka dhibiti/controls za malengo yako.
Fahamu tabia ya taasisi yako inategemea sana namna unavyosimamia kwa umakini ramani yako. Hivyo endelea kujihoji, 'hiki kinachoendelea ndiyo ramani yangu'!? Ikiwa jibu ni 'siyo' chukua hatua za kukiondoa. Na endelea na umakini huo tena na tena maana ndivyo utakavyofikia kilele cha mafanikio yako!

Nimalizie kwa kusema "akili yako ndiyo mafanikio yako" !

Jumamosi, 15 Julai 2017

Vitu vinavyoangusha TAASISI!

Taasisi kushindwa, au kufanya vibaya kama ilivyo kwa mtu mmoja mmoja. Vipo visababishi vya msingi na kwa visababishi hivi, wewe kama kiongozi / mtawala au meneja ni vema ukavifahamu na kuchukua tahadhari ili usishindwe kama hao wengine walivyoshangaa kuona ghafla Taasisi iliyokuwa imara inaanguka kwa muda usiotarajiwa. Visababishi hivyo ni:-
1.kutumia nguvu kubwa na msisitizo mkubwa kwa matokeo ya muda mfupi kwa gharama za utafiti na Maendeleo.
2.kushindwa kutumia fursa na uwezo uliopo, na kushindwa kubaini changamoto dhidi ya Taasisi yako.
3.kupuuzia mbinu za kiutendaji.
4.Kuweka nguvu na msisitizo katika kuzalisha na ubunifu wa kihuduma na siyo zaidi katika ubunifu wa mifumo ya Taasisi pamoja na uboreshaji wa huduma za Taasisi.
5.kupuuzia uwekezaji wa mtaji na rasilimali watu.
6.mawasiliano yasiyo mazuri ndani ya Taasisi na ushirikiano usiomzuri baina ya vitengo ndani ya Taasisi.
7.kutofikiria matarajio na mahitaji ya wateja wa Taasisi. Ufunguo wa mafanikio hapa ni kubainisha mahitaji ya wateja wa Taasisi na kuweka nguvu katika kutimiza matarajio yao. Matarajio ya wateja wa Taasisi ni yapi!? Namna gani tutatimiza matarajio yao!?
Mbinu bora za kiutendaji ni lazima ziende sambamba na kutafuta masoko ya bidhaa ya Taasisi kwa wateja wakubwa na au eneo ambalo Taasisi imeamua kulihudumia.
Kufahamu changamoto mbalimbali zitakufanya meneja, kiongozi/mtawala kubuni mbinu ambazo zinawezekana kabisa kuifanya Taasisi yako iwe hai wakati wote.

Asante,

CEO - "ujasiriamaliafya"

Jumapili, 25 Juni 2017

KUJIKANA, SIFA YA KIONGOZI!

Watu wengi wanapenda kuwa mbele ya wengine yaani kuwa viongozi. Kupenda huko ni jambo jema sana! Mpendwa msomaji wa makala za "ujasiriamaliafya.blogspot.com" kabla ya kutamani kuwa katika nafasi hiyo fahamu kanuni hii "huwezi kwenda juu sana bila kuacha" yeyote aliyefanikiwa kuwa juu sana kwanza alizingatia kanuni hii, "kujikana" Kwa kuacha baadhi ya mambo fulani na kuongeza bidii zaidi katika jambo lile alilolikusudia kwamba litamfanya awe mbele ya wengine.
Kiongozi bora vivyo hivyo ni yule anayeacha mambo yake binafsi na kujitaabisha kwaajili ya wengine. Ataangalia kero na changamoto za wale waliomzunguka au wale anaotaka kuwaongoza na kutafuta njia sahihi ya kuwatoa pale walipo na kuwapeleka kwenye matarajio yao.
Katika mazingira hayo utaona mambo yahusuyo familia yako na mambo yako binafsi yanapewa uzito kidogo kuliko yale ya watu wengine. Dunia ya leo inakosa watu wa namna hii kwa wingi kwani wengi hutamani kuongoza kwa nia ya kujitajirisha au kutafuta faida binafsi.
Jee unatamani kuwa kiongozi bora!? JIKANE NAFSI YAKO NA KUANGALIA YA WENGINE!

KUONGEZA KAMA KANUNI YA UONGOZI

Kiongozi anaongeza thamani katika kuwahudumia wengine.
Ni lazima ujue watu unaotaka kuwaongoza ; ni nini matarajio na matumaini yao!? Ukifahamu hayo unaangalia namna nzuri ya kuwasaidia kuwatoa walipo ili hatimaye wafikie ndoto zao.
Kiongozi husikiliza na kujifunza zaidi ya wale anaowaongoza. Kwa kufanya hivyo ndivyo thamani yako kama kiongozi inavyoongezeka na kukufanya upendwe na kufurahiwa na wale uwaongozao.

UVIVU NA ULEGEVU!!!!

Watu wengi katika maisha ya leo wamekuwa na maisha duni na ya dhiki na kujitumainisha kuwa pengeni ni mapenzi ya Mungu wawe hivyo, hii ni kujifariji na kujitumainisha ndugu yangu katika uongo wa yeye ambaye anapenda uwe ulivyo.
Ndugu yangu na msomaji wa makala za "ujasiriamaliafya.blogspot.com" ni muhimu kufahamu uvivu na ulegevu unaweza kukufanya wakati wote uwe mtu duni na wa chini tu. Mungu aliyetuumba anapenda kutubariki na baraka hizo anasema anabariki kazi za mikono yetu! A haaa kumbe lazima iwepo kazi ndipo kutakuwa na mafanikio!
Nchi yetu ya Tanzania imejaliwa kuwa na mito, na mapori mengi sana ambayo Karibu kila mmoja ni shahidi kwamba kule vijijini kwetu kama yangelitumika vyema bila shaka kila mmoja angekuwa na riziki na kazi ya kufanya.
Hebu fikiria wakati wengine wanaenda shambani kulima wewe unawaangalia tuu! wakati wa mavuno huna mahali pa kuvuna. Haya huyu mke na Mume wanafyatua matofali wajenge nyumba yao, bado wewe unasema kazi ya kufyatua tofali ni kazi duni. Lakini huyu akijitosa kufyatua tofali anauza kiasi ananunua bati na zingine anajengea nyumba yake, wewe bado unashangaa tuu!
Ndugu yangu Zipo fursa nyingi, kinachohitajika ni kuamua kuchukia uvivu na ulegevu na kutamani bidii nakuhakikishia utafanikiwa na utaujutia wakati uliokutangulia.
Umekuwa ulivyo kwasababu kila unalojaribu kufanya unalifanya kwa ulegevu.
Badilika leo na uamue kufanya lolote unaloamini litakutoa kwa bidii na nguvu zote. Miezi sita iliyopo mbele yetu kabla ya kumaliza Mwaka 2017 mambo yatabadilika na historia yako itabadilika kabisa.
Nikutakie mapumziko ya mwisho wa wiki mema.

Jumamosi, 25 Machi 2017

Tafakari ya Robo Mwaka!

Mpendwa msomaji na rafiki yangu wa "ujasiriamaliafya.blogspot.com" kwanza kabisa nikupongeze kwa kufuatilia kwa umakini makala zetu! Nina hakika yapo mafanikio makubwa umeanza kuyaona katika maisha yako kwa hatua yako ya kuwa mtekelezaji wa maarifa hayo na si msomaji tuu! Hongera sana! Lakini Leo tuangalie na kila mmoja ujipime binafsi, tangu mwaka uanze tunakaribia kumaliza robo mwaka. Je shauku na Mipango yako kwa mwaka huu umejitathmini na kuona vinalingana na kalenda ya Mwaka huu kama ulivyokuwa umepangilia Mwanzoni mwa Mwaka au bado kuna vikwazo!? Jee muda wa miezi mitatu, fedha za miezi mitatu, uhai wa miezi mitatu, n.k umevitumia kwa matokeo yanayoonekana na kushikika yaani "tangible"!? Kama jibu lako ni  ndivyo, Hongera sana! Hata hivyo nikukumbushe rafiki yangu, usibweteke kwa yale uliyokwisha fanya tayari bali ongeza jitihada zaidi ili miezi mingine mitatu ijayo tuone tutakuwa tumefikia wapi!? Kumbuka mafanikio ni safari isiyo na mwisho na inahitajika bidii hivyo basi nakushauri endelea mbele huku ukijitahidi kusahau uliyokwisha kuyafanya na kujiona kana kwamba ndio unaanza sasa ndivyoutakavyo fanya makubwa zaidi, kwani hakika tukitumia rasilimali zilizotuzunguka kwa umakini, nina kuhakikishia mambo mazuri zaidi yapo mbele yako!!!