Watu wengi katika maisha ya leo wamekuwa na maisha duni na ya dhiki na kujitumainisha kuwa pengeni ni mapenzi ya Mungu wawe hivyo, hii ni kujifariji na kujitumainisha ndugu yangu katika uongo wa yeye ambaye anapenda uwe ulivyo.
Ndugu yangu na msomaji wa makala za "ujasiriamaliafya.blogspot.com" ni muhimu kufahamu uvivu na ulegevu unaweza kukufanya wakati wote uwe mtu duni na wa chini tu. Mungu aliyetuumba anapenda kutubariki na baraka hizo anasema anabariki kazi za mikono yetu! A haaa kumbe lazima iwepo kazi ndipo kutakuwa na mafanikio!
Nchi yetu ya Tanzania imejaliwa kuwa na mito, na mapori mengi sana ambayo Karibu kila mmoja ni shahidi kwamba kule vijijini kwetu kama yangelitumika vyema bila shaka kila mmoja angekuwa na riziki na kazi ya kufanya.
Hebu fikiria wakati wengine wanaenda shambani kulima wewe unawaangalia tuu! wakati wa mavuno huna mahali pa kuvuna. Haya huyu mke na Mume wanafyatua matofali wajenge nyumba yao, bado wewe unasema kazi ya kufyatua tofali ni kazi duni. Lakini huyu akijitosa kufyatua tofali anauza kiasi ananunua bati na zingine anajengea nyumba yake, wewe bado unashangaa tuu!
Ndugu yangu Zipo fursa nyingi, kinachohitajika ni kuamua kuchukia uvivu na ulegevu na kutamani bidii nakuhakikishia utafanikiwa na utaujutia wakati uliokutangulia.
Umekuwa ulivyo kwasababu kila unalojaribu kufanya unalifanya kwa ulegevu.
Badilika leo na uamue kufanya lolote unaloamini litakutoa kwa bidii na nguvu zote. Miezi sita iliyopo mbele yetu kabla ya kumaliza Mwaka 2017 mambo yatabadilika na historia yako itabadilika kabisa.
Nikutakie mapumziko ya mwisho wa wiki mema.
Jumapili, 25 Juni 2017
UVIVU NA ULEGEVU!!!!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni