Jumanne, 28 Januari 2020

Nioneshe Marafiki Zako nami Nitakuonesha Maisha yako ya Baadaye!

Katika falsafa hii ambayo imezoeleka au inajulikana kwa wengi kama, " ukitaka kujua tabia ya mtu, waangalie marafiki zake".
Marafiki tulio nao sasa wana sehemu kubwa sana katika maisha yetu ya baadaye. Ni kwa namna gani? Wengi wetu na hasa wale wenye imani ya kati au ya juu ya Imani hufikiri kwamba mtu kumpenda ni lazima awe rafiki yako. Mtizamo huu si kweli kabisa! Kuwapenda watu wote kwa kila mchaji wa Mungu ni lazima afanye hivyo. Lakini marafiki siku zote huchaguliwa. Rafiki ni mtu ambaye unaweza kumshirikisha mambo yako ya ndani kabisa naye akawa na mchango katika yale uliyo mshikisha.
Sasa unampataje rafiki? Tafuta namna ya kuwa na urafiki na mtu ambaye unaamini ana kitu fulani ambacho wewe huna na ungependa siku moja wewe nawe uwe nacho, hali kadhalika wewe uwe na kitu fulani ambacho yeye hana. Katika mazingira ya namna ninyi mtakuwa ni marafiki. Hata hivyo fahamu kwamba hakuna ulazima wa wewe kumkumbatia rafiki yako ikiwa unatambua kwa sasa hakuna unachopokea tena toka kwake.
Hii ni kwasababu wenzetu Waamerika hutumia msemo mmoja "hatuna adui au rafiki wa kudumu"
Wewe nawe mpendwa msomaji ukiamua kubadili staili ya maisha na ukazingatia namna ya kumpata rafiki yako mwisho wako utaujua vyema kabisa.
Bila shaka mpaka sasa umekwisha wafahamu marafiki zako, sasa wapime kwa vigezo hivi na imarisha mahusiano na yule unayeamini ana sifa za kumfanya awe rafiki yako.

Asante sana!

Jumatano, 24 Aprili 2019

Soko Huru na Faida Zake.

Soko Huru ni nini!?
Katika hali ya kawaida na inayouchochea uchumi wa eneo lolote ni kuacha bei ya bidhaa ipangwe na soko lenyewe.
Soko linapangaje bei!?
Kwanza mzalishaji huzalisha akitegemea kuuza kwa faida yaani gharama zote za uzalishaji zirejeshwe na ziada. Ukianza kuuza mazao yako pale utakapoona uhitaji wa bidhaa zako ni mkubwa sana ndipo unaongeza uzalishaji ili kuwafanya wateja wako wapate bidhaa yako pasipo shida. Na katika kuongeza uzalishaji pia unaweza kuongeza bei ili kupunguza wateja wasiolazima ili ujue vyema idadi ya wateja wako na ujipange kuzalisha kile kitakachowakidhi wateja hao.
Soko huru husaidia suala la kupunguza bei na au kuongeza bei kuwa chini ya muuzaji na mnunuaji pekee.

Jumapili, 15 Julai 2018

Jee dhamira yako ya mafanikio ni hai!?

Mara nyingi utaona mtu anasema mimi nataka baada ya muda fulani niwe hivi au niwe vile. Na kwa hakika ukisikiliza mawazo na mikakati ya mafanikio utaona mtu huyu ndoto zake ni nzuri sanaa!  Ni kweli kabisa mawazo na ndoto zako zinatia moyo kuzisikia na ni nzuri kweli!
Lakini cha kushangaza utaona siku, wiki,  mwezi na mwaka unapita lakini hakuna kitu kimefanyika waingereza wanasema "no tangible development seen" hakuna maendeleo yanayoonekana.
Nini tatizo!?  Ni muhimu kufahamu bila ya kuwa na moyo wa kujikana na kudhamiria kufikia mipango na malengo yako hakika ndoto na mipango yako itaendelea kuwa ndoto bila kufikia uhalisia wowote.
Jambo lolote ukilipanga na kudhamiria kulifikia nikutie moyo, inawezekana kabisa kwani hata Mungu muumbaji wetu anafanya kazi kwenye bidii yetu, Mithali 10:4 "Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha." Unaona sasa kumbe kinachokosekana ni bidii na kujikana.
Hebu dhamiria sasa bila kuangalia kwamba muda umekwenda sana kwamba bado unaweza kufikia mahali ambapo ikifikia Disemba 2018 utajidharau na kusema ni kweli uliruhusu uvivu na uoga tuu, kwani nakuhakikishia utakuwa umepiga hatua kubwa Kabisa na dhamira ya mipango na ndoto zako utakuwa umevihuisha kabisa!!
Kataa kuwa na ndoto na mipango iliyokufa!!!
Uwe na siku Njema!!!

Jumapili, 25 Machi 2018

111: Kama hakusaidii achana naye!



Mpendwa Msomaji wa makala za “ujasiriamaliafya”, Salaam!
Baada ya salaam napenda leo tuangalie eneo moja la ni yupi rafiki wa muhimu na yupi si rafiki wa muhimu. Kwanza kabisa ni muhimu kufahamu kila binadamu anayo thamani kubwa sana kwa kuwepo kwake hapa duniani ingawa si kila binadamu anaweza kuwa rafiki yako. Neno rafiki au kiingereza “friend” ni mtu ambaye kwa namna yeyote atakuwa ni mtu wako wa karibu katika furaha na huzuni. Atakuwa ni mtu anayependa kukuona unafanikiwa na kuendelea mbele. Na hapa haijalishi kwamba unalingana naye umri au ni mdogo kuliko wewe au mkubwa kuliko wewe.
Rafiki anaweza kutoka katika kundi lolote iwe kazini, katika eneo lako la biashara au mahali popote, muhimu kuangalia jee anakidhi vigezo vya kuwa mtu wangu wa karibu katika dhiki au katika furaha au mawazo yake yananifanya nisonge mbele!???. Fahamu jambo moja hapa rafiki kwa vigezo tunavyoangalia leo ni zaidi ya ndugu, mke au mume wako.
Watu wengi utaona wanatunza namba nyingi sana katika simu zao na utaona hata kuzipoteza hawako tayari, kwamba wacha niwe nazo tuu. Swali la kujiuliza jee namba za simu zote ulizozitunza ni za marafiki zako au watu baki tuu!? Kuwa na kundi kubwa ambalo kimsingi siyo marafiki zako ni kujichelewesha kimaendeleo na kupoteza muda wako ambao kama ungeutumia vizuri matokeo yangekuwa yakushangaza.
Ili uweze kwenda kwa kukimbia na siyo kutembea, leo ninakushauri achana na marafiki wasikuwa wa msaada kwako kwani hao ni mizigo inayokufanya usikimbie katika mafanikio yako na zaidi waweza kurudishwa nyuma.
Leo tuchukue muda wa kutafakari umuhimu wa kila unayemuita rafiki yako na kama hakusaidii mfute na mpotezee kwani hakusaidii!!! Ili kufikia mafanikio makubwa na malengo ambayo umekuwa ukiota ndoto ya kuyafikia wakati wote, muhimu ni kupunguza marafiki wasio na msaada kwako. Na baada ya kuwapunguza imarisha na ongeza nguvu kubwa zaidi ya kuwashikilia hao wachache ambao umetambua ya kuwa ndio marafiki zako.
Nakutakia siku njema!
Mtega GFA
CEO – UjasiriamaliAfya

Jumapili, 4 Februari 2018

Mafanikio sio kitu Rahisi!

Ndugu na Rafiki yangu mpendwa salaam!
Ni matumaini yangu kwamba bado upo katika mapambano ya kufikia kile kizuri unachokitaka.
Wengi wetu tumekuwa tukisoma katika vitabu au nadharia mbalimbali zinazotuongoza katika kufikia mafanikio.
Leo hii napenda nikwambie maneno ambayo yumkini hutayapenda sana lakini ndio ukweli wenyewe.
Kufikia mafanikio siyo rahisi kama tunavyosoma nadharia mbalimbali. Viko vizuizi vingi vya kukukatisha tamaa na kukuvunja moyo ili kuhakikisha hufiki kule unako taka ufikie. Hebu mfano angalia jinsi usingizi ulivyomzuri lakini upande wa pili ukilala bila utaratibu fahamu ndoto za mafanikio zitabaki kuwa ndoto. Hapa ni lazima kuudhibiti usingizi. Wataalam wanatufundisha masaa ya kulala kwa afya ni sita pekee, je mwenzangu unalala masaa mangapi kwa siku!?  Hapa nikuombe uchukue hatua ya kuudhibiti usingizi na uutumie muda wako vizuri! 
Tambua kuwa usingizi ni kizuizi kimojawapo cha mafanikio ingawa upande wa pili usingizi ni mzuri sana.

.........Kwa leo tuishie hapo na tutaendelea wakati ujao.

Mtega GFA
CEO - UjasiriamaliAfya

Jumatatu, 1 Januari 2018

Ni MWISHO WA YOTE!!

Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala za UjasiriamaliAfya, UjasiriamaliAfya blog tunakutakia "Heri ya Mwaka Mpya 2018" lakini kwa nini kila tunapomaliza mwaka huwa tunapeana na kutumiana salaam za heri ya Mwaka Mpya!?
Ndugu msomaji ni muhimu kufahamu ni kwa nini kuna masaa,siku,wiki,mwezi na hatimaye mwaka!?  Ni makusudi ya Mungu muumbaji wetu kuwepo nyakati na majira,  na majira na nyakati zikipita kinakuja kitu kingine kipya kabisa!
Sasa kwa kuanzia hapa sisi nasi leo tutumie muda kidogo kutafakari majira na nyakati. Mwaka 2017 ndio unaishia na inawezekana kuna mipango na mambo mengi ulipanga yafanyike lakini sasa unaona dakika zimebaki kidogo na hakuna matumaini tena.
Hebu fahamu nyakati ngumu, nyakati za huzuni, nyakati za kutofanikiwa na nyakati za machungu sasa zimekaribia kuishia na 2017 yake.
Unachotakiwa kufanya sasa chukua karatasi na kalamu yako kisha orodhesha mipango na mikakati unayotaka kuiendea mwaka 2018 kwani huo mwaka 2018 ni zawadi kwetu na mambo ni mapya kabisa.
Tangu mapema sahau kushindwa kwako kwa 2017 na tambua 2018 ni nafasi mpya tumepewa. Ukianza bila mipango utaufunga mwaka bila tathimini.
Kumbuka nidhamu ya kujituma, na bidii zaidi katika mipango yako ya 2018.

2018 na uwe wa heri na mafanikio makubwa makubwa kwako!!!!!!

Asante sana!

Mtega George
CEO - UjasiriamaliAfya