Mara nyingi utaona mtu anasema mimi nataka baada ya muda fulani niwe hivi au niwe vile. Na kwa hakika ukisikiliza mawazo na mikakati ya mafanikio utaona mtu huyu ndoto zake ni nzuri sanaa! Ni kweli kabisa mawazo na ndoto zako zinatia moyo kuzisikia na ni nzuri kweli!
Lakini cha kushangaza utaona siku, wiki, mwezi na mwaka unapita lakini hakuna kitu kimefanyika waingereza wanasema "no tangible development seen" hakuna maendeleo yanayoonekana.
Nini tatizo!? Ni muhimu kufahamu bila ya kuwa na moyo wa kujikana na kudhamiria kufikia mipango na malengo yako hakika ndoto na mipango yako itaendelea kuwa ndoto bila kufikia uhalisia wowote.
Jambo lolote ukilipanga na kudhamiria kulifikia nikutie moyo, inawezekana kabisa kwani hata Mungu muumbaji wetu anafanya kazi kwenye bidii yetu, Mithali 10:4 "Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini;Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha." Unaona sasa kumbe kinachokosekana ni bidii na kujikana.
Hebu dhamiria sasa bila kuangalia kwamba muda umekwenda sana kwamba bado unaweza kufikia mahali ambapo ikifikia Disemba 2018 utajidharau na kusema ni kweli uliruhusu uvivu na uoga tuu, kwani nakuhakikishia utakuwa umepiga hatua kubwa Kabisa na dhamira ya mipango na ndoto zako utakuwa umevihuisha kabisa!!
Kataa kuwa na ndoto na mipango iliyokufa!!!

Uwe na siku Njema!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni