Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa makala za UjasiriamaliAfya, UjasiriamaliAfya blog tunakutakia "Heri ya Mwaka Mpya 2018" lakini kwa nini kila tunapomaliza mwaka huwa tunapeana na kutumiana salaam za heri ya Mwaka Mpya!?
Ndugu msomaji ni muhimu kufahamu ni kwa nini kuna masaa,siku,wiki,mwezi na hatimaye mwaka!? Ni makusudi ya Mungu muumbaji wetu kuwepo nyakati na majira, na majira na nyakati zikipita kinakuja kitu kingine kipya kabisa!
Sasa kwa kuanzia hapa sisi nasi leo tutumie muda kidogo kutafakari majira na nyakati. Mwaka 2017 ndio unaishia na inawezekana kuna mipango na mambo mengi ulipanga yafanyike lakini sasa unaona dakika zimebaki kidogo na hakuna matumaini tena.
Hebu fahamu nyakati ngumu, nyakati za huzuni, nyakati za kutofanikiwa na nyakati za machungu sasa zimekaribia kuishia na 2017 yake.
Unachotakiwa kufanya sasa chukua karatasi na kalamu yako kisha orodhesha mipango na mikakati unayotaka kuiendea mwaka 2018 kwani huo mwaka 2018 ni zawadi kwetu na mambo ni mapya kabisa.
Tangu mapema sahau kushindwa kwako kwa 2017 na tambua 2018 ni nafasi mpya tumepewa. Ukianza bila mipango utaufunga mwaka bila tathimini.
Kumbuka nidhamu ya kujituma, na bidii zaidi katika mipango yako ya 2018.
2018 na uwe wa heri na mafanikio makubwa makubwa kwako!!!!!!
Asante sana!
Mtega George
CEO - UjasiriamaliAfya
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni