Jumanne, 28 Januari 2020

Nioneshe Marafiki Zako nami Nitakuonesha Maisha yako ya Baadaye!

Katika falsafa hii ambayo imezoeleka au inajulikana kwa wengi kama, " ukitaka kujua tabia ya mtu, waangalie marafiki zake".
Marafiki tulio nao sasa wana sehemu kubwa sana katika maisha yetu ya baadaye. Ni kwa namna gani? Wengi wetu na hasa wale wenye imani ya kati au ya juu ya Imani hufikiri kwamba mtu kumpenda ni lazima awe rafiki yako. Mtizamo huu si kweli kabisa! Kuwapenda watu wote kwa kila mchaji wa Mungu ni lazima afanye hivyo. Lakini marafiki siku zote huchaguliwa. Rafiki ni mtu ambaye unaweza kumshirikisha mambo yako ya ndani kabisa naye akawa na mchango katika yale uliyo mshikisha.
Sasa unampataje rafiki? Tafuta namna ya kuwa na urafiki na mtu ambaye unaamini ana kitu fulani ambacho wewe huna na ungependa siku moja wewe nawe uwe nacho, hali kadhalika wewe uwe na kitu fulani ambacho yeye hana. Katika mazingira ya namna ninyi mtakuwa ni marafiki. Hata hivyo fahamu kwamba hakuna ulazima wa wewe kumkumbatia rafiki yako ikiwa unatambua kwa sasa hakuna unachopokea tena toka kwake.
Hii ni kwasababu wenzetu Waamerika hutumia msemo mmoja "hatuna adui au rafiki wa kudumu"
Wewe nawe mpendwa msomaji ukiamua kubadili staili ya maisha na ukazingatia namna ya kumpata rafiki yako mwisho wako utaujua vyema kabisa.
Bila shaka mpaka sasa umekwisha wafahamu marafiki zako, sasa wapime kwa vigezo hivi na imarisha mahusiano na yule unayeamini ana sifa za kumfanya awe rafiki yako.

Asante sana!

Hakuna maoni: