Mpendwa msomaji wa makala za ujasiriamaliafya, hebu leo tuangalie namna "uongozi unavyoendelea" Ni muhimu kama mjasiriamali kufahamu Uongozi ni Maendeleo ya kila siku na si Maendeleo ya siku moja Pekee! Hii ina maana unaweza ukajua mtu mwisho wake kwa kusoma tabia yake ya kila siku na vipaumbele vyake. Kama Kiongozi ni lazima uwe na mpango binafsi wa maendeleo yako. Maxwell anaandika "ni kitu gani unachokiona kwa mtu pale unapoangalia mipango yake ya kila siku? vipaumbele, mwamuko, uwezo, mahusiano, mtizamo, nidhamu binafsi, maono, na mvuto wake" vitu vyote hivi uvionavyo ndio hasaa vinachangia kujua nini utakuwa mwisho wa safari ya maisha yake. Kwahiyo basi kwa kuangalia hayo haijalishi unataka uwe nani au mwisho wako uweje? ikiwa hutaamua sasa njia unayotaka kuipitia au kuielekea. Kwani kila jambo linahitaji maandalizi na mipango katika kulifikia.
Kanuni hii pia inakuja pale tunapokuwa viongozi wa wengine, kama wewe ni kiongozi bila shaka utakuwa unahitaji maendeleo na mafanikio katika uongozi wako! basi fanya hivyo kwa wale unaowaongoza pia ili waweze kuwa na mwisho wenye mafanikio na maendeleo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni