Ushawishi ndicho kipimo kikuu cha Uongozi wako! Je umewahi jiuliza swali hili, "ni nani ninayemshawishi!?"
Inawezekana swali kubwa tukajiuliza, Ni ushawishi wa namna gani tunautoa kwa wale wanaotufuata? Viongozi wasiojiamini mara nyingi hupenda kuwafanya wale wanaowaongoza wawe chini wakati wote ili kulinda nafasi zao katika makundi wanayoyaongoza. Hii ni aibu.Viongozi wazuri mara nyingi utaona wanatambua kuwa kazi yao kubwa ni kuwainua wanyonge na kuhakikisha wanatoka katika unyonge wao na kuwa juu hata kama siku moja itatokea wakawa juu zaidi kupita Kiongozi mwenyewe.
Uongozi si mpaka uitwe jina kubwaa kwani uongozi haupatikani kwa kuwa na jina kubwa au cheo kikubwaa, kama wewe ni Mtendaji Mkuu, Mchungaji, Mkurugenzi, Meneja, au Mtu Mkubwa katika Nyumba bado wewe hujawa kiongozi ikiwa wale unaosema unawaongoza bado hawafuati maongozi yako. Maxwell anasema, "uongozi wa kweli haupatikani kwa kutunukiwa,au kupewa na mtu au kupangiwa na mtu" uongozi unakuja kwa kuwa na ushawishi kwa wengine, ndio maana hauji kwa kupewa na mtu au kupangiwa na mtu. Ni kitu kinachokuja toka ndani mwa mtu. Anaendelea kusema, "ukitaka kumtambua kiongozi wa kweli usisikilize mtu anayejipambanua mwenyewe kuwa kiongozi, usipime kwa kuangalia vile alivyonavyo, usiangalie cheo chake au jina lake. Angalia ushawishi alio nao kwa wengine na ushuhuda utauona kwa wale wanaomfuata au waamini wake". Na anamalizia kwa kusema "yule anayefikiri anaongoza lakini hana wanaomfuata ni sawa na mpita njia".
Jumatano, 20 Septemba 2017
Ushawishi chanya ndicho kipimo cha Uongozi.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni