SOMO: KWA NINI ELIMU YA KINA YA UJINSIA,
MAADILI YA AFYA NA STADI ZA MAISHA [Comprehensive Sexuality Education – CSE]?
Ø Inawawezesha
Vijana balehe kujizuia na mimba zisizotarajiwa na maambukizo kwa njia ya ngono,
ikiwa ni pamoja na VVU.
Ø Inawasaidia
Vijana balehe kufanya maamuzi sahihi hasa ya kuchelewa kuanza kufanya ngono na
ukatili wa kijinsia.
Ø Ina
hamasisha Vijana balehe kuwa na uhusiano unaofaa zaidi na wenye Afya pamoja na kupunguza ukatili wa
kijinsia, uonevu na ubaguzi.
KWA
NINI HUDUMA ZA UJINSIA NA AFYA YA UZAZI – Sexuality Reproductive Health?
Vijana balehe
wanahitaji kupata elimu salama, za gharama nafuu na zinazokubalika kulingana na
viwango vya Kimataifa vya Huduma Rafiki za Afya ya Uzazi kwa Vijana.
Serikali zinawajibu wa kutoa huduma hizi kwa
sababu:
Ø Kutimiza
haki ya afya ya umma kulinda afya ya kizazi kijacho.
Ø Zitolewe
kwa pamoja na huduma nyingine za elimu ya ujinsia, afya ya uzazi, maadili ya
afya na stadi za maisha zenye ufanisi zaidi.
Ø Kuhakikisha
kwamba Vijana balehe wanajisikia salama na kujiamini katika upatikanaji wa
huduma.
Ø Kupunguza
mimba zisizotarajiwa, VVU, magonjwa mengine ya ngono na kuboresha kiwango cha
kuishi kwa wajawazito na watoto
hatimaye kuliletea Taifa letu maendeleo makubwa sana.
VIJANA WA LEO.
HALI
HALISI YA AFYA YA UZAZI KWA VIJANA TANZANIA
VIJANA
NI
IDADI KUBWA YA WANANCHI TANZANIA
UJANA
ni
umri kati ya miaka 10 hadi 24. Ni kipindi cha mpito kati ya utoto na utu uzima
ambapo vijana wanapitia mabadiliko mengi ya ukuaji na kiafya.
RIPOTI
YA TAFITI ZA DEMOGRAFIA NA AFYA ZA 2010.
·
Tanzania ilikuwa na jumla ya watu milioni
43.2 [ 43,187 823 ], Vijana milioni 14 = 31%
MATATIZO YA VIJANA YA AFYA YA UZAZI
1.
Wasichana wengi huanza kujihusisha na
ngono kwa wastani wakiwa na umri wa miaka 17 wakati wavulana miaka 15
2.
Vijana wengi huanza kujihusisha na
mapenzi kabla ya kuingia kwenye ndoa.
3.
32% ya wasichana wasioolewa na wavulana 42% wasiooa wa umri wa miaka 14 -20 walishaanza kujamiana.
4.
9% ya wasichana na 10% ya wavulana wa
miaka 15 – 20 walishaanza kujamiana kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.
5.
Inakadiriwa kuwa 65% ya wasichana wafikapo umri wa miaka 18
tayari huwa wameshaanza kujamiiana.
6.
18% ya wasichana wenye umri wa
miaka 15 – 19 tayari wameshaolewa na
37% ya wasichana wenye umri wa miaka 20 – 24
waliolewa au kuwa kwenye unyumba
walipokuwa na umri wa miaka 18.
7.
4% ya wavulana wenye umri kati ya
miaka 15 -19 wameshaoa. Ndoa za utotoni hutokea kwa kiwango kikubwa katika
Mikoa ya Shinyanga ambapo 59% ya wasichana wenye umri wa miaka 15 -19 walishaolewa
na mkoa wa Mara ni 55%.Kuolewa katika umri chini ya miaka 20 ni kuwaweka
wasichana katika hatari ya kupata mimba za utotoni.
Ø Mimba
katika umri mdogo ni tatizo kubwa mojawapo la Afya ya Uzazi hapa nchini.
Ø 23%
ya wasichana wenye umri wa miaka 15 – 19 wamekwisha zaa watoto hai au wana
mimba ya kwanza ambapo 6% wana ujauzito wa kwanza.
Ø Wasichana
116 kati ya 1000 wenye umri kati ya miaka 10 – 19 wana watoto tayari.
Ø Ni
16% tu ya wasichana wenye umri wa miaka 15 – 24 wanatumia njia za kisasa za
uzazi wa mpango.
Ø 22%
ya wasichana wanataka kutumia njia za uzazi wa mpango lakini wanashindwa kupata
huduma hizo.
WASICHANA KUPATA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO
v Ni
tatizo kubwa sana la afya ya uzazi nchini.
v 23%
ya wasichana wenye umri wa kati ya 15 -19 wamekwisha zaa mtoto hai au wana
mimba.
v 52%
ya wasichana wenye umri wa miaka 15 -19 hawana elimu ya sekondari kutokana na
kuapata mimba ama watoto.
v Mimba
za utotoni huchangia vifo vingi vya wajawazito na watoto.
v Watoto
waliozaliwa na wasichana wenye umri mdogo wananafasi ndogo
ya kuishi kufikia miaka 5 ikilinganishwa na wale wanao zaliwa na wanawake wenye umri mkubwa.
v Wasichana
111 kwa 1000 wenye umri chini ya miaka 20 hupoteza watoto wao tofauti na vifo
vya watoto waliozaliwa na wanawake wenye umri
kati ya miaka 30 hadi 39 ambapo ni 93 kwa 1000.
UTOAJI MIMBA.
Vifo
ni 16%, wengi wao ni vijana.
MATATIZO YA KUJAMIIANA KATIKA UMRI MDOGO.
Kwa Msichana
A.
Kukatiza
masomo na kuathirika kimaisha.
B.
Kukataliwa
na familia.
C.
Kupata
matatizo wakati wa kujifungua.
D.
Kifo
Kwa Mvulana:
A. Kukatiza
masomo na kuathirika kimaisha.
B. Kufunga ndoa
za kulazimishwa.
C. Kukosa uwezo
wa kulea familia.
Kwa mtoto:
Ø Kuzaliwa na
uzito pungufu.
Ø Kuzaliwa mtoto
njiti.
Ø Kupata
matatizo wakati wa kuzaliwa
Ø Kukosa mapenzi
kwa wazazi.
Ø Kifo
VIJANA NA
MAAMBUKIZO YA VVU/UKIMWI
v UKIMWI ni ugonjwa unaosababishwa na Virusi
Vya UKIMWI [VVU/ HIV] vinavyodhoofisha kinga ya mwili ya kujikinga na maradhi
mbalimbali.
JINSI UKIMWI
UNAVYOENEZWA.
Ø 90%
ya maambukizo ni kwa njia ya kujamiiana na mtu mwenye VVU.
Ø Mama
mwenye VVU anaweza kumwambukiza mototo wake wakati wa:
a.
Ujauzito.
b.
Uchungu na kujifungua.
c.
Kunyonyesha
d.
Kuchangia damu yenye VVU.
ü Karibu
1/2 ya wasichana na 1/3 ya wavulana wamewahi kupimwa VVU na kupokea majibu yao.
ü Vijana wa miaka 15 – 24 huchangia kwa 2% ya
maambukizi mapya ya VVU Tanzania.
ü Vijana
walio kwenye ndoa au wanaishi na wenza maambukizi ya VVU ni 2.6% ikilinganishwa
na 1.4% ya ambao hawako kwenye ndoa.
ü Maambukizi
mapya ya VVU ni 45% kwa wasichana wenye umri kati ya miaka 15 – 24 wakati
wanaume ni 26% kwa umri huo.
ü Magonjwa
ya ngono yanaongeza kasi ya maambukizo ya VVU.
MAGONJWA
YATOKANAYO NA KUJAMIANA.
Magonjwa
yanayo ambukizwa kwa njia ya tendo la kujamiiana na mtu ni miongoni mwa magonjwa haya;
Ø Kisonono
Ø Klamidia
Ø Trichomoniasis
Ø Kaswende
Ø Herpes
Ø Pangusa
– Chancroid
Ø Virusi
Vya UKIMWI
NAMNA YA KUJIKINGA NA MIMBA.
v Kuacha
kabisa kujamiana.
v Tumia
kondomu kila wakati na kwa usahihi.
v Tumia
njia ya uzazi wa mpango uliyoichagua kuzuia mimba.
NAMNA
YA KUEPUKA TENDO LA KUJAMIIANA AMBALO SI SALAMA NA SI LAZIMA KWA WASIO NA NDOA.
ü Epuka
kujamiiana katika umri mdogo, kama ulishaanza acha mara moja.
ü Epuka
ulevi wa aina yoyote ile
ü Shiriki
katika michezo mbalimbali ili kupambana na mihemko ya mwili wako.
ü Endapo
utashindwa kujizuia kabisa unashauriwa kutumia kondomu kwa usahihi.
ü Kondomu
ikitumika kwa usahihi kwa kila tendo la kujamiiana huzuia mimba, maambukizo ya
VVU na magonjwa ya ngono.
ü Epuka
kushirikiana na rafiki mpenda ngono,kuomba omba/ kupewa zawadi mbalimbali na vishawishi
vingine vingi ambavyo vitasababisha uingie katika ngono.
ü Usifanye
rushwa ya ngono, ni kosa la kisheria.
ü Epuka
tabia ya uvivu.
ü Usishiriki
michezo na mikesha ya usiku isiyo ya lazima.
ü Enzi
Mafundisho ya dini yako kwani ni mafundisho yanayo kataza zinaa.
TAHADHARI kwa Wasichana:
Wanaweza kupata mimba
v Kabla
ya kupata hedhi.
v Bila
kufanya tendo la kujamiiana endapo katika hali ya mapenzi mvulana atamwaga shahawa karibu na UKE.
v Wanapofanya
tendo la kujamiiana kwa mara ya kwanza.
NJIA ZA UZAZI WA MPANGO:
a]
Za muda mfupi:
> Vidonge vyenye Vichocheo Viwili
> ,, ,, kichocheo kimoja [POPS]
> Dawa Za Povu Na Jeli [Spermicides]
> Njia ya Ute [BOM]
> Kunyonyesha Tu [LAM]
b]
Za muda mrefu:
> Sindano [ Depo Provena ]
> Vipandikizi [ Norplant ]
> Kitanzi [ IUCD ]
AFYA
YA UZAZI NA MALEZI KWA VIJANA BALEHE.
C]
Njia za kudumu:
> Kufunga uzazi mwanaume [
Vasectomy ]
> Kufunga uzazi mwanamke [ BTL
]
Marejeo:
1. Youth in
Tanzania – data from the 2010 Tanzania Demographic and Health Survey ( TDHS ).
2. Vijana Wa Leo
handouts – Wizara ya afya na U/Jamii.
3. National
Adolescent Reproductive Health Strategy 2011 – 2015.
4. Wizara ya Afya
na U/Jamii, Kitengo Cha Afya ya Uzazi na Mtoto, barua pepe:Afya_promo@moh.go.tz
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni