Theodore Roosevelt aliwahi kusema "mtendaji mzuri ni yule anayetambua watu makini na kuwachukua wafanye kile anachohitaji kifanyike na bila kuwaingilia wakati wanafanya kile anachotaka kifanyike"
Maxwell anasema hii ni kwasababu "kuwaacha watu wabakie katika hali ya chini ni lazima wewe uliye juu uamue kuishi maisha ya chini na katika kufanya hivyo unakuwa unapoteza uwezo wako wa kuwainua wale walio chini"
Maxwell anaendelea kusema "kiukweli kuna nguvu katika uwezeshaji si kwa mtu yule anayetaka kutoka katika hali yake duni bali hata kwa mwezeshaji mwenyewe, katika kumuinua aliye duni inakufanya na wewe uinuke zaidi" katika falsafa hii tuna kitu cha kujifunza leo kama kanuni ya maisha yetu ya kila siku kwamba tunapotengeneza viongozi au watendaji wazuri katika jamii na familia pia si tuu kwamba tunajiongezea thamani lakini thamani ya Taasisi tunazotumikia zinajiongezea thamani kupitia mchakato huu.
Asante na nikutakie Siku Njema!
CEO - www.ujasiliamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni