Jumapili, 19 Februari 2017

Marafiki na Maisha yako ya Baadaye!

"ukinionyesha marafiki zako, nitakuonyesha maisha yako ya baadaye"  au "show me your friends, I will show you, your future"

Mpendwa rafiki yangu naomba nikushirikishe falsafa hii ambayo hutumiwa sana na washauri mbalimbali. Maisha yetu ya baadaye yanategemea sana marafiki wetu wa sasa.

Haihitajiki muujiza au utabiri kujua maisha yako ya baadaye yatakuwa ya namna gani!? Je marafiki ulionao sasa wanakupa changamoto za kujiandalia maisha yako ya baadaye kiroho na kimwili chako!?
Kama marafiki ulio nao sasa wanaendekeza anasa au hawawazi lolote la maisha ya baadaye, ninakushauri ni vema ukachukua hatua ya kuachana nao na kuwatafuta marafiki ambao watakupa wivu wa kutamani mafanikio kwaajili ya maisha yako ya baadaye na kukutia moyo ili hatimaye mipango yako na ndoto zako uziendee kwavitendo sasa!

Uwe na siku njema!

Hakuna maoni: