Katika maisha yetu ya kila siku, utaona kama kuna jambo lolote haliendi vile unavyotaka watu wengi huanza kulaumu au kunung'unika kwaajili ya fulani.
Ni muhimu kufahamu moyo wa mtu yeyote unapaswa kuwa kama moyo wa mfanya biashara. Ili bidhaa zako ziweze kuuzika unapaswa kuwa na nguvu ya kuwashawishi wale unaotaka wanunue bidhaa yako kwa kuwaeleza nini kilicho cha ziada ikiwa wataamua kununua au kutumia bidhaa zako.
Katika eneo hili hunabudi kutumia Mbinu bora za mawasiliano ili usikilizwe.
Na pia fahamu si kila unayekutana naye lazima akusikilize, wapo watakao kukebehi, kukuvunja moyo, n.k hapo ndipo kwenye mtego. Jitahidi unapokutana nayo yasikuyumbishe na kukutoa kwenye lengo kuu! Ukifanikiwa katika eneo hili ninakuhakikishia utauza bidhaa zako na utastawi sana!
Nikutakie siku njema!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni