Jumapili, 19 Februari 2017

"Ukitaka kung'aa kama jua.... "

"ukitaka ung'ae kama jua, kwanza uungue juani" au "if you want to shine like a sun, First burn like a sun".  By Dr. Kalam

Mafanikio yeyote yaliyo halali kwahakika hayana urahisi. Watu wengi hupenda mafanikio ya kimwili au ya kiroho tena haraka haraka! 

Ndugu yangu Usidanganyike! Wahenga walisema "usione vyaelea,  vimeundwa"

Jambo lolote unaloliona ni zuri sasa wako watu waliokubali kuumia na kuteseka na hayo kimsingi ni matokeo yake. Ikiwa unataka ung'ae kama jua kwanza kubali uunguzwe kwa moto mkali wa jua.

Hapa nina maana kwamba mafanikio yanahitaji kujikana na kuachana na mambo yote yasiyo na tija sasa na ukiyaacha hayo unaweza kuwakosa marafiki na mambo mazuri mengi sasa.

Lakini ukidhamiria, ninakuhakikishia utanga'a kama jua na kila mmoja atakutamani. Dhamiria na jiamini kwamba safari bado ni mbichi kabisa. Jipe moyo, fanya jambo hilo kwa bidii yako yote, na akili yako yote, na nguvu zako zote!  Kwahakika unakwenda kung'aa kama Jua!

Uwe na siku njema!

Hakuna maoni: