"Hakuna mafanikio pasipo Kujikana"! Kila unayemuona amefanikiwa kwa lolote fahamu kuna mambo aliyaacha na akatumia bidii kubwa katika jambo hilo mwisho tunasema na kushuhudia kuwa amefanikiwa!
Watu wengi hushindwa kufikia ndoto zao za mafanikio kwa kuwaza kuwa mambo ni rahisi tuu! Ndugu yangu Usidanganyike! Kila jambo zuri unaloliona kwa mtu na kulitamani, fahamu mtu huyo alikubali Kujikana.
Kiongozi mzuri pia ni yule mwenye moyo wa kuwatanguliza wale anao waongoza, ataamini uongozi wake utakuwa bora ikiwa atadumu kutenda kazi katika timu. Kadhalika atayapa uzito na kutoa majibu ya malengo binafsi ya wale anaowaongoza, akijua wale anaowaongoza wapo pale katika taasisi yake ili kutimiza ndoto zao binafsi katika maisha.
Mwisho nikutake ndugu msomaji ufanye yafuatayo;
weka nguvu zako zote katika lile unalolifanya na kamwe usiangalie vikwazo katika jambo hilo, ushindi kwahakika ni lazima!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni