Chama cha Akiba na Kukopa
Chama cha akiba na mikopo ni kikundi cha watu waliojiunga kwa hiari yao kufanya ushirika wa kuweka akiba zao kwa pamoja na kutoa mikopo kwa urahisi kutokana na akiba zao.
Chama cha akiba na mikopo ni kikundi cha watu waliojiunga kwa hiari yao kufanya ushirika wa kuweka akiba zao kwa pamoja na kutoa mikopo kwa urahisi kutokana na akiba zao.
Kwa wafugaji wa kuku kibiashara wanashauriwa kuwa na chombo cha namna hii kitakachokuwa na utaratibu wa wanachama kuweka na pia wanachama hawa kuwa na fursa ya kukopa kwa lengo kubwa la kuendeleza ufugaji wao kuku kibiashara.Ufugaji wa kibiashara ungehitaji kuongeza mtaji mara kwa mara kulingana na mahitaji ya soko husika. Mfumo wa kuweka na kukopa utakuwa chanzo kizuri na cha kuaminika kukidhi haja ya mtaji endelevu kwa wafugaji wa kuku.
Michango kwa ajili ya akiba inaweza kutokana na makato ya mapato yanayotokana na mauzo ya bidhaa za kuku ( vifaranga,mayai, kuku n.k. ). Au kiwango maalum kwa wakati maalum kinaweza kuwekwa na wanachama ili kitolewe kwa utaratibi wanaokubalianana. Wanachama wanaweza kukopa kutoka kwenye chama chao kwa ajili ya ununuzi wa mahitaji,mbalimbali ya kuku kama:
- Madawa
- Vyakula
- Ukarabati au ujenzi wa mabanda ya kuku n.k
Faida za chama kama hiki ni:
- Wanachama watapata sehemu ya kuhifadhi pesa yao kwa usalama kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
- Masharti ya kukopa ni nafuu kuliko vyombo vingine vya kifedha.
- Wanachama hujifunza misingi ya kushirikiana, mahusiano na kusaidiana.
- Wanachama hupata maarifa ya ziada kuhusu maswala ya kifedha.
Chama cha namna hii, lazima kiwe na kanuni za kukiongoza ambazo hutungwa na wanachama wenyewe.
Kanuni hizi zilenge kulinda malengo ya chama na kila mwanachama anawajibika kuzizingatia.
Mambo makuu ya kuzingatia katika katiba ni:
- Malengo ya chama
- Haki, wajibu na malengo ya wanachama
- Viwango vya viingilio
- Hisa na michango
- Uongozi na majukumu
- Vikao na mikutano
- Utunzaji wa kumbukumbu
- Mikopo na riba
- Taratibu za kutoa mikopo
- Migawanyo ya faida
Mambo ya msingi ya kusimamia na kuendesha chama cha Akiba na Kukopa ni pamoja na:
- Uhiari wa wanachama
- Uongozi uwe wa kidemokrasia
- Kusiwe na urasimu
- Chama lazima kiwe na vitabu vitakavyotumika kuweka kumbukumbu ya hifadhi za fedha za wanachama
- Uwekaji wa akiba uwe wa mara kwa mara
- Mkopo ulipwe kwa muda uliopangwa
- Fedha za chama ziwekwe benki au kwenye masanduku maalum ya kutunzia kwa utaratibu uliopendekezwa Mahesabu ya chama yafanyiwe ukaguzi mara kwa mara.
Kikundi kama hiki kinaunganisha nguvu pamoja na kupunguza tatizo la kupata huduma ya kifedha hasa katika maeneo ya vijijini.Hata hivyo jambo la msingi la kufanikisha malengo ya vyombo hivi ni kuzingatia kanuni zilizowekwa na wahusika. Vilevile utaalam wa kutosha wa kuendesha na kusimamia chombo vya namna hii ni muhimu uwepo.
Source: RLDC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni