Jumatano, 14 Desemba 2016

Utunzaji wa Kuku

Ulishaji
Kuku kama mifugo mingine uhitaji chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ili kukua upesi na kuwa na na afya nzuri . Chakula kinachofaa ni mchanganyiko wa viini lishe mbalimbali vyenye kazi tofauti mwilini. Kila kiini lishe hakina budi kiwe katika kiwango sahihi kulingana mahitaji ya mwili wa kuku katika umri tofauti. 

Kuku anahitaji chakula chenye viini lishe vifuatavyo:

Kiini lishe
Kinapatikana katika chakula gani
Kazi yake mwilini
Wanga
Pumba,Chenga za nafaka kama
mahindi, mtama.
Kutia nguvu mwilini
Mafuta
Mashudu yanayopatikana baada ya
kukamua mbegu za mafuta kama
alizeti, karanga n.k
Kutia nguvu na joto
mwilini
Protini
Mashudu ya karanga au alizeti.Damu
iliyokaushwa ya wanyama kama
mbuzi, ng’ombe n.k. Mbegu za jamii
ya mikunde kama maharage, kunde,
soya....
Kujenga mwili na
kukarabati mwili
Vitamini
Majani mabichi kama mabaki ya
mboga za majani, michicha ya porini,
majani mabichi ya mipapai, majani ya
Lusina n.k.
Kulinda mwili. Majani
mabichi pia huwezesha
kuku kutaga mayai yenye
kiina cha njano, rangi
ambayo huwavutia walaji
wengi.
Madini (calsium
na Fosforas)
Unga wa dagaa, unga wa mifupa
iliyochomwa, chokaa
Kujenga mifupa,
kutengeneza maganda
ya mayai

Mfano wa kuandaa vyakula vya makundi tofauti ya kuku
 
Kwa Vifaranga

Kwa vifaranga vya tangu kutotolewa hadi miezi miwili tengeneza mchanganyiko ufuatao.Huu ni mfano mmojawapo wa kuandaa kilo 100 za chakula cha vifaranga. Iwapo utahitaji kuandaa jumla ya kilo 50 za chakula tumia nusu ya vipimo vilivyoainishwa katika jedwali hili.
 
Wastani wa mahitaji ya kuku wakubwa 50 kwa siku ni kilo 5. Chakula hiki ukigawe katika sehemu mbili na kuwapatia nusu asubuhi na nusu ya pili mchana.
 
Vifaranga hupewa chakula kiasi wanachoweza kumaliza (hawapimiwi).

Vifaa
Kiasi kwa kilo
Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
12 hadi 15
Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
40
Mashudu
20
Pumba
24
Chokaa
2
Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
2
Chumvi
Robo kilo
Mchanga
1
Jumla
Kilo 100

 Kwa kuku wanaokua (baada ya miezi miwili ).

Vifaa
Kiasi kwa kilo
Dagaa (unga au vichwa vya dagaa)
7
Chenga za nafaka kama mahindi au mtama n.k
30
Mashudu
20
Pumba
39
Chokaa
2
Unga wa Mifupa,Madini ( Premix)
2
Chumvi
Robo kilo
Mchanga
1
Jumla
Kilo 100

Kama umeamua kufuga kuku kwa mtindo wa kuwaacha huru wajitafutie chakula (huria) unaweza kuwapatia vifaranga nyongeza ya protini.Utafanya hivyo kwa kuwachanganyia vumbi au vichwa vya dagaa kiasi cha kikombe kimoja vilivyotwangwa pamoja na pumba ya mahindi vikombe vitano.
 
Maji ya Kunywa
Mfugaji ahakikishe anawapatia kuku maji masafi ya kunywa na ya kutosha kila siku.Vyombo vya maji ya kunywa budi visafishwe vizuri kila siku. Hii itasaidia sana kudhibiti magonjwa yanayoweza kutokana na vimelea vya magonjwa vinavyostawi katika maji yasiyo safi. Kuku wanaweza kuwekewa maji katika aina tofauti ya vyombo kutegemea na urahisi wa kupatikana mfano sufuria, ndoo za plastik zilizokatwa kuruhusu kuku kunywa bila kuchafua.
 
Usafi katika banda
Matandazo yanayowekwa katika sakafu ya banda la kuku hayana budi yageuzwe mara kwa mara kwa wastani wa kila baada ya miezi miwili au mitatu . Wakati mwingine ni kabla ya kipindi hiki muda wowote yanapoloana na maji. Matandazo uharakisha kukauka kwa unyevu katika banda unaotokana na kinyesi cha kuku na pia zaidi na maji yanayomwagika.
 
Usafi katika banda utasaidia kudhibiti kwa kiasi kikubwa magonjwa mbalimbali.
 
Kuokota mayai
Usiyaache mayai ndani ya viota kwa muda mrefu, yaokote mara kwa mara ili kuepuka kuharibiwa kwa mayai hayo na kuku wenyewe. Kuku wanayo tabia ya kula mayai yao ikiwa chakula unachowapa kina upungufu wa protini.
 
Vilevile kiasi cha mwanga unaoingia ndani ya banda kikizidi kuku hula mayai au kudonoana wenyewe kwa wenyewe.Uonapo dalili za namna hii kwenye kundi lako punguza kiasi cha mwanga kwa kuziba sehemu za madirisha kwa vipande vya magunia au vipande vya makasha ya karatasi ngumu.
 
Kama ilivyoelezwa awali kuku wapewe majani mabichi ya kutosha mara kwa mara ili wawe wanakula hayo badala ya kudonoana. Pia fuatilia kuhakikiksha kama chakula kina protini ya kutosha. Kama tatizo la kudonoana na kula mayai litaendelea omba msaada kwa mtaalam wa mifugo akuelekeze jinsi ya
kuwakata au kuwachoma midomo.
Source: RLDC

Hakuna maoni: