Alhamisi, 15 Desemba 2016

Magonjwa ya Kuku

Magonjwa ya Kuku
Magonjwa ya kuku yapo mengi. Hata hivyo siyo yote yanatokea mara kwa mara hapa Tanzania. IIi uweze kudhibiti yale yanayotokea katika kundi lako unahitaji kufahamu dalili za jumla za magonjwa hayo. Unapoigundua moja au zaidi ya dalili za ugonjwa au wadudu chukua hatua mara moja. Yapo magonjwa ambayo yanaweza kuangamiza kundi lote la kuku katika muda mfupi.
 
Jihadhari na uwezekano wa kupatwa na hasara zinazoletwa na magonjwa ambayo unaweza kuyazuia.
 
Katika sehemu hii utajifunza kwa muhtasari tu dalili za jumla za magonjwa ya kuku na jinsi ya kuyadhibiti.

Dalili za Jumla za Magonjwa ya Kuku
  • Kuku kupoteza hamu ya kula.
  • Kuzubaa na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu (Kutochangamka).
  • Kushuka kwa kiwango cha utagaji wa mayai.
  • Vifaranga kutokua upesi au kudumaa. - Macho kuwa na rangi nyekundu.
  • Kujikunja shingo.
  • Kutetemeka, kutoa majimaji puani, mdomoni na machoni.
  • Kutoa mharo (kinyesi) wa rangi ya kijani au wenye mchanganyiko na damu au cheupe.
  • Kukonda.
  • Kukohoa.

Ukiona moja au zaidi ya dalili hizi katika kundi lako chukua hatua za kutibu zilizoelezwa hapa chini. Kama hali ni ngumu zaidi omba msaada kwa mtaalam wa tiba ya mifugo ili achunguze mara moja na kukushauri jambo la kufanya. 

Muhtasari wa Magonjwa Muhimu ya Kuku na Jinsi ya Kuyadhibiti na Kutibu

Ugonjwa
Chanzo
Dalili
Kudhibiti na Kutibu
1. Kideri
(Newcastle)
Virusi
Kukohoa, kupumua
kwa shida.
Mwili
kukosa nguvu; shingo
kujikunja.
Kuharisha kijani.
Kuku hufa wengi
Kuhara damu.
Vifaranga wachanjwe
katika juma lao la
kwanza. Chanjo la pili
wanapofikisha umri wa
miezi 4 na nusu.
Chanja kuku kila baada ya
miezi mitatu.
2. Kuhara damu
(Coccidiosis)
Bakteria
Kuku hujikusanya pamoja.
Hawachangamki.
Hushusha mbawa.
• Tunza usafi katika
banda.
• Lisha vifaranga chakula
k i l ichochanganywa
na dawa ya kinga
coccidiost kama
Amprolium au Salfa.
• Watenge kuku wote
Walioambukizwa na
wapatie dawa kama
Amprolium au salfa au
Esb3.
3. Ndui ya kuku
(Fowl pox)
Virusi
Malengelenge kwenye
kishungi na kope za
macho na sehemu zisizo
na manyoya.
• Kuchanja kuku wote
wakiwa na umri wa
miezi miwili.
• Watenge kuku wote
walioambukizwa na
wapewe antibiotic kama
OTC plus au salfa.
4. Mafua ya kuku
(Fowl coryza)
Bakteria
Kuku uvimba uso na
macho
Kamasi hutirirka puani na
mdomoni
Kuhema kwa shida hata
kukoroma.
Kukohoa.
• Usafi wa banda
• Kuchanja kuku wote
• Kabla hawajaambukizwa
kama ni tatizo sugu
katika eneo
• Watibu wanaougua
kwa kutumia anti biotic
kama sulphamethazine,
streptomycine na
vitamin
5. Kuharisha
nyeupe
Bakteria
Kuharisha nyeupe na
hamu ya kula kupungua.
Wadudu washambuliao
Kuku
• Usafi wa vyombo na
banda kwa ujumla
• Watenge kuku
wagonjwa
• Tumia dawa kama
Furazolidone au
Sulfadimidine
• Hata vitunguusaumu menya robo
kilo utwange nu
kuchanganya na
maji lita moja. Chuja
uwapatie maji haya kwa
muda wa wiki moja.
Wadudu washambuliao Kuku
Viroboto,Chawa,
Papasi

Kuku hawatulii, hujikuna
mara kwa mara.
Hupungukiwa na damu na
uzito
Wadudu huonekana
mwilini
Wadudu washambuliao
Kuku
Usafi wa banda na
mazingira
Banda lipitishe hewa ya
kutosha ili liwe kavu
Nyunyizia kuku na banda
zima dawa za kuua wadudu
kama vile Akheri powder,
Malathion, Servin n.k
 
Kutoa chanjo ya kideri kwa njia ya kuweka
matone ya dawa katika macho
 Njia kuu za ujumla za kudhibiti magonjwa ni:
  • Kutunza hali ya usafi ndani ya banda na kudhiditi kusiwe na unyevu
  • Matandazo yakichafuka yabadilishwe.
  • Vyombo vya maji visafishwe kila siku
  • Jitahidi uepuke kufuga kwa njia ya huria ili kuku wako wasiambukizwe magonjwa kirahisi
  • Epuka kufuga kuku wako pamoja na bata na khanga.Hawa ni wabebaji wa vimelea vya magonjwa ya kuku japo wao hubaki
    salama.
  • Zingatia ratiba za chanjo kwa magonja yasiyo na tiba kama kideri na mengineyo ya virusi
Source: RLDC

Hakuna maoni: