Alhamisi, 15 Desemba 2016

Kusimamia Ufugaji Wako

Kutunza kumbukumbu
Ili ufanikiwe katika ufugaji wa kuku, ni muhimu sana kulifahamu vyemi kundi la kuku wako. Ukilifahamu vema kundi lako utaweza: 

Kuchagua kuku bora wa kuzalishia kwa kuangalia ubora wa wazazi wao. Kufahamu historia ya afya ya kundi, kwa mfano
  • Umri ambapo vifaranga vilipata chanjo.
  • Ni chanjo ya aina gani.
  • Magonjwa ambayo yamewahi kushuambulia kundi, na dawa ulizotumia katika matibabu.
  • ldadi ya kuku wanaokufa.
  • Kukadiria kiasi cha chakula ambacho kuku wako watahitaji kwa muda fulani na aina ya chakula.
  • Kujua kila siku kuku wametaga mayai mangapi.
  • Kujua utahitaji muda gani kutunza kuku toka vifaranga mpaka wanapofikia kuuzwa.
Ili uweze kufahamu mambo haya yote unahitaji kutunza kumbukumbu Ufuatao hapa chini ni mfano rahisi wa kutunza kumbukumbu za kuku tangu wangali vifaranga mpaka wanapofikia uzito wa kuuzwa.

Mfano wa Kumbukumbu za ufugaji wa Kuku


Kumbukumbu ya Vyakula
Tarehe
Kiasi cha Chakula
(Kilo)
Kundi / Umri wa
kuku na idadi yao
Maoni (Gharama,
Kimetumika kwa muda gani n.k.)

15
Vifaranga






25
Wanaokua

Jumla





Hapa utaweza kujua wastani wa matumizi ya chakula kwa idadi ya kuku na kwa kipindi husika.
Tarehe ya kuuza……………………….
Idadi iliyouzwa……………………………
Umri wa kuku wakati wa kuwauza................
Mapato kutokana na kuuza……………………


Kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
Magonjwa
Tiba
Maoni (vifo, gharama nk)
3.7.2016
coccidiosis
teramycin

5.9.2016
mdondo
furazolidone











Kumbukumbu hii itakusaidia kujua magonjwa yanayosumbua mara kwa mara na kwa kipindi kipi. Pia na dawa inayosaidia zaidi kwa tatizo husika.


Chanjo au Kudhibiti magonjwa
Tarehe
Ugonjwa/Wadudu
Dawa
Gharama
6.8.2016
Viroboto
Kunyunyiza doom powder au sevin powder

5.10.2016
coccidiosis
Amprol katika maji, kinga dhidi ya











Jinsi ya Kufahamu Faida Unayopata
IIi uweze kufahamu faida unayopata kutokana na ufugaji wa kuku inakupasa kutunza kumbukumbu za matumizi na mapato ya kila siku.

Kwa mfano:

Upande wa matumizi ingiza
  • Gharama ya kununua vifaranga (kama walitotolewa hapo hapo nyumbani inafaa ukadirie gharama hiyo).
  • Gharama ya chakula.
  • Kama unatengeneza na kuchanganya wewe mwenyewe kadiria kwa kutumia bei za viungo ghafi.
  • Gharama ya mafuta ya taa (kama uliwakuza vifaranga kwa joto Ia taa).
  • Gharama ya kusafisha banda kubadili matandazo.
  • Gharama za madawa ya kinga (chanjo) na tiba.
Upande wa mapato ingiza mapato kutokana na:
  • Mauzo ya mayai.
  • Mauzo ya kuku hai.
  • Gharama ya mayai yaliyotumiwa nyumbani.
  • Mauzo ya mbolea kutoka katika banda.
Ufuatao ni mfano unaoonyesha jinsi ya kuingiza taarifa hizi katika daftari la kumbukumbu


Kumbukumbu ya Kutibu Magonjwa
Tarehe
Matumizi
Sh.
Tarehe
Mapato
Sh.

Kununua vifaranga
30 @ 200/=
6,000/=

Mauzo ya mayai 10
@150/=
1,500/=

Kununua vyakula
kilo 10 @150/=
1,500/=

Mayai na kuku
waliotumiwa
nyumbani
7,000/=

Dawa ya kukohoa
1500/=
Dawa ya
1,500/=

Mauzo ya kuku 20
@ 4000/=
80,000/

Dawa ya wadudu
1000/=
1000/=

Mbolea iliyouzwa


……nk.
……nk.

……nk.
……nk.
Jumla







Baada ya kufanya mauzo yote ya kundi jumlisha matumizi yote na jumlisha na mapato yote katika kipindi kizima cha kufuga. 

Ili kufahamu faida uliyopata fanya hesabu hii:

Jumla ya Mapato yote - Jumla ya Matumizi yote = Faida

Source RLDC

Hakuna maoni: