Jumanne, 29 Novemba 2016

NA.191 - NA.195: ISHI MAISHA RAHISI!



191. Jitahidi kuwa mtu uliye wazi. Uwe mwaminifu binafsi na hata watu wengine wakuamini.
192. Nguvu ya kutaka kwako itaongezeka sana kama ukidhibiti maneno yako. Mtu anafungwa na kitu fulani kizuri, huingia katika ugumu sana na kukosa furaha ikiwa kitu hicho kitatoweka. Watu wenye furaha wakati wote ni wale ambao hufurahia jambo lolote pasipo kukubali kufungwa na jambo hilo. Ishi maisha rahisi, ya utaratibu, na kujibidiisha katika uzalishaji. Katika kurahisisha maisha nyakati hizi waza kuuza runinga yako, acha kufuatilia meseji zisizo na tija, uwe na matumizi ya wastani, waza kuuza gari yako, jifunze kutulia na kutafakari kila asubuhi na ondoa mlio katika simu yako unaoweza kukutoa katika kutafakari.
193. Kama hujacheka katika siku ya leo; fahamu leo hujaishi. Cheka sana na kwa nguvu kama William James alivyosema, "we don't laugh because we are happy, we are happy because we laugh." Akimaanisha “hatucheki kwasababu tunayo furaha, tuna furaha kwakuwa tunacheka”.
194. Soma kitabu kiitwacho, “The Charisma Factor”  Namna gani unaweza kuendeleza uwezo wa kiasili katika uongozi kama kilivyotolewa na Robert J, Richardson na S. Katherine Thayer. Ni kitabu kizuri sana kwa kila anayetaka kuwa kiongozi bora au tayari ni kiongozi na unataka kupiga hatua zaidi katika uongozi wako.
195. Safiri mara kwa mara. Kwani kutembelea katika eneo jipya ambalo hujawahi tembelea ni jambo la msingi sana na inakuruhusu kutambua na kubainisha fursa ambazo vinginevyo usingezipata.

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: