Jumatano, 30 Novemba 2016

NA.196 - NA.200: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.




196. Kila mwezi jiwekee malengo katika kuimarisha afya yako. Mfano unaweza kuanza na mazoezi ya uogeleji au vinginevyo. Lengo likiwa ni kufikia pale ulipokusudia katika mwezi, andika hilo kwa kumbukumbu na uwaze kufanya tena na tena.
197. Mara zote vitu huumbwa kwa namna mbili. Upo uumbaji unaoanzia kwenye akili na uumbaji wa kiuhalisia yaani unaweza kuona na kugusa. Kama ilivyo mipango ya nyumbani kwamba kwanza utaanza kuiweka katika maandishi kabla ya utekelezaji. Vivyo hivyo na mipango yako ya siku inapaswa kuanza kabla ya machweo. Fikiria maajabu ambayo unapenda yawe sehemu katika maisha yako na utashangaa inakuwa hivyo kadiri unavyosonga mbele. Hii ni sawa kabisa kiuasili.
198. Nenda kazini na tambua uzuri na ajabu katika mazingira ya asili..
199. Lala kidogo, matumizi yako yawe ya chini, fanya kazi kwa bidii, utaishi muda mrefu na kuwa mtu mashuhuri.
200. Mwisho endelea kusoma mfululizo huu tena na tena na kuwashirikisha wengine!


Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa makala za "ujasiriamaliafya" tunapenda kukupongeza kwa ufuatiliaji ulio makini katika kipindi chote ambacho tumekuwa tukitoa makala hizi na hatimaye leo tunahitimisha. Hata hivyo muhimu kufahamu hapa ni kwamba kazi iliyokuwa inafanywa ilikuwa ni kuujenga msingi ambao utatumika sasa katika makala zifuatazo kujenga nyumba. Bila shaka ukifuatana nasi hali yako ya kutokufanikiwa na kukwama kwama itabadilika kabisa ikiwa tutauzingatia msingi huu ulio katika mfululizo wa siri 200 za kufanikiwa katika maisha. Hivyo tujitahidi kuyatendea kazi.
Nahitimisha siku hii ya leo kwa kukutakia ujenzi mwema na endelea kufurahia "ujasiriamaliafya" kwa vitu moto moto mbalimbali vitakavyoendelea kuwekwa kwenye ukurasa wetu huu.


\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: