Jumatatu, 28 Novemba 2016

NA.186 - NA.190: AKILI NI KAMA BUSTANI.



186. Jaribu kula matunda na maziwa tuu kwa siku nzima. Watu wa mashariki ya mbali wamemudu kuimarisha afya zao kupitia mbinu ya kufunga au kuacha kula vyakula vigumu na kula vyakula laini. Kwa kufanya hivyo baada ya wiki kadhaa utagundua kuimarika kwa nguvu za mwili wako tofauti na awali na wepesi katika kutembea. Chakula kizuri kinahitaji kuwa na virutubisho ambavyo utahakikisha vinachanganywa wakati wa maandalizi ili kuimarisha afya yako.
187. Thamini furaha ya mshirika wako na kumjengea picha kwamba unathamini kazi yake kila siku.
188. Ikiwa una mwenzi, jitahidi kuzitunza kumbukumbu za kuoana kwenu wakati wote.
189. Akili ni kama bustani, ukipanda basi utavuna. Unapojiendeleza na kuijali akili yako, itastawi kwa kiwango usichotarajia. Bali ukiacha magugu yaitawale akili yako kamwe hutafikia malengo yako. Chochote unachokiingiza kwenye akili yako ndicho kitakachotoka katika akili yako. Kwahiyo epuka kuangalia sinema, vitabu vya simulizi mbaya, na vitu vyote visivyofaa au vyenye mtizamo hasi. Watu mashuhuri katika mafanikio ni watu waliochagua kwa umakini vitu vya kuingiza katika akili zao kabla. Kwa hakika huwezi kupata faraja kutokana na fikra hasi.
190. Tabia ya kukaa na kusimama kwa siku mara nyingi zaidi ni nzuri katika kuimarisha misuli yako itakayokufanya mwisho wa siku uifurahie afya yako na kuwa na uhakika nayo. Hii pia inatengeneza maumbile yako na kukuongezea kujiamini zaidi.

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: