Jumapili, 27 Novemba 2016

NA.181 - NA.185: MAISHA SI UJANA NI AKILI.



181. Angalia kielelezo cha tabia ya kiwango cha juu kabisa:
             Umakini na uhakika katika mawazo na maelezo.
             Mwenendo wa kuyachuja mambo na upole.
             Uwezo na tabia ya kuyapima mambo kabla ya kuyatendea kazi.
             Uwezo wa kujiendeleza mwenyewe pasipo kutegemea mtu fulani.
             Uwezo wa kufikia malengo uliyojipangia na ndoto za maisha yako.
182. Maisha si ujana ni akili. Watu wanazeeka kutokana na mawazo wanayo kuwa nayo na mawazo hayo huwatoa kabisa katika hali ya ujana. Miaka inafanya ngozi ijikunje, lakini ukiwa unaiwazia sana inafanya moyo ukunjamane pia. Utazeeka kulingana na mawazo na wasiwasi ulionao, woga wako, msongo wa mawazo na uzembe. Njia ya kutunza ujana wako ni kujiamini na kuwa na uhakika ya kwamba wewe ni kijana wakati wote. Tumaini lako liwe ni ujana.
183. Chunguza dawa za kichina na zile za kutoka mashariki kama zitakufaa kwa kuweka mwili wako tatika afya bora na ni vema kushauriana na matabibu ili upate ushauri stahiki kabla ya kuanza kutumia kulingana na matatizo uliyo nayo ya kiafya.
184.  Tumia muda wako vizuri katika vipaumbele vyako kila siku kwa kufanya kwanza mambo ya msingi katika maisha yako.Ni rahisi kusema hapana wakati ndiyo inaonekana kutawala ndani mwako.
185. Usiwe na haraka katika maisha. Katika miaka tuliyonayo tunatakiwa kuendesha maisha yetu kwa utulivu. Zingatia  kile ambacho ni muhimu na  ufanye shughuli ambazo hazitakufanya uwe na haraka na ambazo zitarudishia  uasili wako na zitakufanya uwe na amani. Kaa kwenye majani na angalia anga kwa muda wa nusu saa na hili siyo rahisi kama watu wanavyofikiri. Ushauri wangu ni kukufanya upate muda wa mapumziko kwa muda mfupi ukifurahia utulivu.
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: