Alhamisi, 24 Novemba 2016

NA.176 - NA.180: WAFURAHIE MAJIRANI ZAKO.



176. Ijaze nyumba yako mwanga na maua mazuri ya asili. Hii ni aina ya uwekezaji ambao waweza kufanya. Weka muziki mzuri na tulivu ndani ya nyumba yako ili iwe sehemu nzuri kwa ajili ya mapumziko.
177. Ni vema kuwafahamu na kuwafurahia majirani zako. Watafanya maisha yako kuwa mepesi na kukupa msaada pale unapohitaji.
178. Tambua nguvu ya kuimba na mwangwi wake, maneno yenye hamasa na nguvu. Wahindi hutumia njia hii kwa takribani miaka 4000 ili kuwaletea maisha ya utulivu na maendeleo makubwa.  Tengeneza wimbo wako mwenyewe ambao utauimba kwa kurudia rudia kila siku katika kuimarisha tabia yako na kukujengea moyo wa nguvu.
179. Akili inafanya kazi yake vizuri pale kunapokuwa na utulivu katika upumuaji.
180. Tumia taswira ifuatayo siku kwa siku. Keti mahali palipotulia na tafakari picha ya namna unavyotaka uwe katika maisha yako. Utakuwa mtu wa namna gani, utaitwaje na utakuwa unafanya nini? Maswali hayo yatakupa undani wa vitu gani hujavikamilisha na unapaswa kuvikamilisha ili ufikie hatua hiyo.
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: