171. Kumbuka
kununua mfuko wa mpango ambao utahakikisha kuwa una chombo kizuri cha kuratibu,
kutunza mipango yako na majukumu uliyonayo katika maisha yako kwa utaratibu
mzuri.
172. Jisomee
vitabu mbalimbali kila baada ya miezi michache ukitafuta hazina katika ujenzi
wa tabia kupitia waandishi wa vitabu hivyo. Utajifunza namna ya kuzungumza
mbele ya watu wengi kwa usahihi, utabadilika kitabia na kuwa na tabia njema
sana, matumizi mabaya ya muda utayaacha, utakuwa na afya nzuri na vitu vingine
vingi sana utajifunza kwa gharama ndogo. Utagundua miongoni mwa vitabu hivyo
vya zamani ni vizuri sana katika kujenga tabia na nidhamu ya katika maisha.
173. Soma
kitabu kiitwacho “The Magic of Believing” kilichoandikwa na Claude M.Bristol. Kitakufundisha
namna ya kukabili nguvu ambazo mara kwa mara zilikuwa zikikufuatilia lakini
hazikuwa na faida kwako.
174. Tamani
kujulikana kama mtu mtulivu, mwenye moyo mzuri na tabia njema. Uwepo wako hapa
duniani utakumbukwa kwa muda mrefu hata baada ya kuondoka kwako.
175. Inaaminika
kwamba kufanya jambo kwa ajili ya wengine ni imani ya juu sana. Katika wiki
moja kuna masaa168 tunayoyatumia, tumia masaa machache kuwahudumia wengine.
Wengi wanaamini ukiacha ubinafsi na kuwahudumia wengine baada ya muda mfupi
utashangaa inakuwa ni sehemu katika maisha yako. Tumia muda wako kwa wazee
wasiojiweza au kwa watoto yatima. Fundisha jinsi ya kusoma au namna ya
kuzungumza mbele ya watu wengi na kwa matendo hayo utakuwa umewaachia urithi
mzuri sana.
Kwa
leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni