166. Kutumia
muda katika kufanya maendeleo yako binafsi ni kitu cha msingi sana, usijaribu
hata kidogo kupoteza mda wako kwa kufanya mambo yasiyo muhimu. Kuchukua saa moja
kwa masaa ya asubuhi kuangalia watoto wadogo wanaocheza karibu au kutembea
polepole ukiwa unaenda mahali fulani ni kupoteza muda. Lakini kwa kutumia muda
wako vizuri itakusaidia sana kufanya shughuli zako za uzalishaji binafsi vizuri
na hivyo kujiletea maendeleo. Huwezi kufanya vizuri kama hujisikii vizuri.Ukiwa
na utulivu mzuri waweza fanya vizuri sana shughuli zako za uzalishaji, pia waweza
kuwa mbunifu na kuwa mtu unayeendana na mazingira.
167. Soma
kwa bidii, jifunze kwa bidii, cheka sana na uwe na upendo zaidi. Hii
itakusaidia kuwa na uchangamfu katika moyo wako.
168. Chagua
aina tano za mahusiano ambayo unapenda yatakayo kufanya upande ngazi baada ya
miezi sita ijayo. Andika majina ya hao watu ambao unataka kuimarisha mahusiano
nao na kila jina moja andika maelezo kwa nini unapenda kuimarisha mahusiano, namna
ya kuimarisha mahusiano na kwa muda gani? Huu ni uwanja wa pekee wa kupanga
malengo yako. Ni zoezi ambalo litakuletea majibu mazuri sana katika kila uwanja
wa kutafuta mafanikio yako. Jiandae kuwa mzazi bora, rafiki mzuri na raia bora.
Kuwa mbunifu katika hatua unazochukua kuonesha kwamba umekubaliana nao na
unawaheshimu wapendwa wako. Kuwapa taarifa ni vizuri lakini kumbuka utofauti na
vipimo vya mawazo yao na umbali kutoka mahali walipo mpaka sehemu ambayo
mnakwenda kukaa pamoja na kufurahia.
169. Kumbuka
nguvu ya maombi juu. Maombi ni silaha kubwa kuliko silaha zote tuzijuazo
duniani katika kutupatia mema tunayoyahitaji.
170. Uwekezaji
mzuri katika ukuaji wako binafsi unapatikana kutoka kwenye mafundisho ya kaseti
sita ya Reverend Dr.Norman Vincent Peale yaitwayo "The Power of Positive
Thinking”. Pata nakala hizo na sikiliza tena na tena. Ndani yake kuna mikakati
na mbinu ambazo zitakufanya usiwe mtu wa kushindwa, bali zitakufanya shughuli
zako ziishi muda mrefu, ukiwa ni mwenye furaha, na maisha ya kustawi.
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni