161. Kila siku fanya vitu viwili ambavyo ulikuwa
hupendi kuvifanya. Hii itakuwa ni maandalizi ya taarifa ambayo umekuwa ukiiweka
pembeni. Usiangalie ni jambo dogo kiasi gani wewe fanya tuu! Baada ya muda
mfupi utaanza kuona shughuli hizo zilizokuwa zinaonekana hafifu kwako si hafifu
tena, na bidii yako binafsi itaongezeka na matokeo yako yataongezeka. Jaribu
kufanya hivyo kwani hii ni mbinu ya zamani ambayo ilitumika na watu mbalimbali
katika kujenga nguvu ya tabia.
162. Furaha
ya kweli hutokana na kitu kimoja: mafanikio ya malengo, iwe ya binafsi,
kitaalamu au vyovyote. Unakuwa na furaha pale unapohisi unaongezeka. Pale
unapohisi kwamba mchango wako unakupeleka katika ndoto zako, utajihisi kuwa na
nguvu zisizo kifani na shauku kubwa. Kuutumia muda katika jambo ambalo malipo
yake ni kidogo kutokana na kuacha kujisikia katika kujifurahisha mfano kuangalia
Runinga ni muda unaoupoteza na hauwezi kuupata tena. Kujifurahisha ni muhimu
lakini tafuta namna ya kuufidia muda huo na shughuli za uzalishaji ambazo
zitakupelekea kufikia malengo yako ya mafanikio. Furaha huja kwa kutenda na si
kulala.
163. Huko
Ufaransa, Napoleon wa Tatu alikuwa na uwezo wa kukumbuka majina ya watu wote
aliokutana nao. Siri kubwa ilikuwa ni kusema “samahani sana, nikumbushe majina
yako” kila alipokutana na mtu ambaye hajawahi kutana naye. Hii inafanya jina
kujirudia rudia na kulazimisha kukaa katika kumbukumbu. Na kama jina lilikuwa
gumu, aliomba litamkwe kwa alfabeti kikamilifu.
164. Msingi
wa wa-China umejengwa juu ya falsafa hii katika maisha takribani miaka maelfu
sasa: kujijenga katika roho ya ujasiri, heshima na uadilifu. Kadiri unavyo
rudia rudia kujiweka katika hali hiyo ndivyo unavyokuwa mtu wa kipekee
unayeheshimika na wengi. Tumia bidii yako kuona kwamba wewe nawe unapata sifa
hiyo.
165. Mbinu
pekee ya kukabili fikra kinzani zinapokuja kwako kwa nia ya kukukatisha tamaa
na kukuzuia kuyaendea mafanikio ni kuwa na nyenzo ya kuyazuia mawazo na akili. Mawazo
ya kushindwa yanapoingia kwako kwanza hunabudi kujitambua na kutamani kuyaondoa
kwa kutumia fikra za kushinda mara moja. Unaweza kutamka kinyume chake kwani
mawazo na akili husikia unapotamka mfano “mimi ni jasiri” au “mimi naweza”
kadiri unavyotumia ulimi wako vizuri dhidi ya fikra hasi ndivyo fikra hasi zitakavyotoweka
na fikra chanya zitatawala ndani mwako.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni