156. Hakikisha
kazini kwako unajulikane kama mtu mbunifu. Kaa chini na andika mawazo kumi
kwenda kwa kiongozi wako ambayo utajadiliana naye juu ya kuboresha kazi zako na
ubora wa eneo lenu la kazi kwaujumla. Jiweke katika hali itakayo kutambulisha
kuwa mtu mwenye mawazo yanayobainisha changamoto na namna ya kuzishughulikia
kwa umakini na shauku kubwa.
157. Moyo
uliochangamka ni dawa nzuri! Hivyo jifunze kucheka peke yako.
158. Madirisha
ya akili yako yaache wazi wakati wote na kujiweka tayari kupokea mawazo tofauti
tofauti ambayo ni kama fursa kwako kuchagua ufanye lipi na uache lipi.
159. Jaribu
kwenda siku moja nzima bila kusema nitafanya bali lenga kupokea toka kwa
wengine. Sikiliza toka kwa wengine na kwa hakika utajifunza vitu vingi vipya na
vya ajabu sana na zaidi kujiongezea marafiki.
160. Tumia
saa moja katika siku kwa ukimya kabisa isipokuwa kujibu maswali mojakwa moja.
Hata hivyo jibu swali utakalo ulizwa moja kwa moja bila kutaka kuendeleza mazungumzo.
Ni kawaida ya binadamu kuzungumza kitu kwa kurudia rudia. Kama wahenga wa mashariki wafanyavyo si tu
itakujengea nguvu ya kuhiari bali itakujengea kueleweka kwa wepesi na lugha ya
inayoonesha umakini ambayo ni muhimu kwa mawasiliano ya uhakika.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni