151. Kila
aliyefanikiwa na kupata matokeo makubwa juu ya jambo analolifanya, kwanza
alijijengea matumaini makubwa ndani yake kabla ya kufikia hatua hiyo. Pasipo matumaini
mwelekeo wa maisha hupotea na ugumu hutokea katika kila hatua unayopiga.
Matumaini ni tabia ya muhimu katika maisha.
152. Hebu
leo orodhesha tabia saba nzuri unazotamani zingekuwa katika maisha yako alafu
zibandike karibu kabisa na kitanda chako. Alafu kila asubuhi lenga kwenye tabia
moja tuu ambayo utahakikisha katika siku yako unaitekeleza. Baada ya wiki moja
utagundua mabadiliko kidogo katika maisha yako. Ndani ya mwezi mmoja utabaini
kuyafanya vizuri yote. Ndani ya miezi miwili tabia zote saba zitakuwa zako.
153. Unazo
sifa nyingi kadiri unavyofanya mambo yako na watu wengi tofauti tofauti kwani
kila mmoja hukufikiria tofauti kabisa. Kitu cha msingi hapa kuangalia na kujali
ni tabia yako mwenyewe halisi. Unaouwezo kamili wa kumiliki au kuisimamia tabia
yako, jichunguze na kujijengea tabia njema. Kama tabia yako ni njema na
unasimamia hilo. Kila mwenye mtizamo chanya juu yako atapenda kukufuata au
kwenda na wewe.
154. Chukulia
wewe ni chungwa. Kile kilicho halisi ndani yako ndicho kitakutoka. Kama akili
yako imejaa mawazo ya utulivu, mtizamo chanya, nguvu, ujasiri na huruma, kama
mtu akija kwako hiyo ndiyo juisi itakayo kutoka ndani yako.
155. Maisha yetu
hayaelezewi katika umilele jinsi itakavyokuwa. Tupo lakini ni kama katika hatua
ndogo sana katika sayari hii. Kama ijulikanavyo hatutachukua chochote
tunapoyaendea maisha hayo ya milele, basi maana halisi ya uwepo wetu hapa ni
kutoa na kuhudumia wengine. Jitahidi kuwa hivyo wakati wote. Unapoamka asubuhi
na mapema tamka maneno haya ya kujitega mwenyewe: “leo nitahudumia wengine,
nitawajali watu leo na nitakuwa mwema pia”. Aina hii ya maisha itakulipa malipo
mengi kama ukidumu katika kusudi la kuwasaidia wengine badala ya kuwaza
kujinufaisha wewe mwenyewe binafsi.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni