146. Jenga tabia ya kufanya
shughuli sahihi kwa wakati sahihi na mahali sahihi, hii itakusaidia kuwa na
mafanikio makubwa.pia hii itakufanya kuwa na nidhamu kwa wenzio na kuonesha
unawajali sana. Bila hii kila mtu atakuona hufai. Usiwahi sana na usichelewe
sana, pangilia muda wako na uwepo eneo la tukio mapema kama mlivyokubaliana na
wenzio ili uwe na utulivu. Kwa kufanya hivyo tabia iliyo adimu kwa wengi utakubalika
na kila mtu popote utakapoenda na kukaribishwa vizuri na kupendwa sana.
147. Simu
ipo kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano yako sio kwa ajili ya wengine
wanaotaka kuwasiliana wewe.Kama umetingwa sana na kazi usijibu simu yoyote
ambayo umepigiwa subiri muda utakao kuwa huna kazi na umetulia kabisa ndipo
uwasiliane na huyo mtu.Usiruhusu muingiliano wa mawazo wakati wa kazi, utapoteza
muda.Mara nyingi simu zinazopigwa huwa hazina mambo ya msingi ya kuzungumzia na
hupoteza muda mwingi sana kwa kuongea. Watu wengi wamekosa mafanikio na kupoteza
muda wao kwa kutumia muda mwingi kuongea na simu badala ya kufanya kazi
zitakazo waongezea kipato.
148. Uianze
siku yako vizuri. Kabla ya kukiacha kitanda chako kila asubuhi, mshukuru Mungu
kwa kukuamsha salama wewe na familia yako, pia mwambie asante kwa kuiona siku
mpya na kwa kila kitu kizuri alichokupa wewe na familia yako. Anza kuiona hiyo
siku ni nzuri sana kwako na itakuwa ya
furaha, mafanikio na utulivu kwako. Na kama unaamini hayo hakika ndivyo
yatakavyokuwa. Siri ya matumizi mazuri ya muda wako ni kuona kila siku kama ni
nafasi ya kipekee na haitakuja tena
149. Jitahidi
kumshirikisha mambo yako mwenzi wako. Kwa kufanya hivyo mahusiano yenu
yataimarishwa na kuwafanya mwende kwa kasi ya pamoja. Kushirikishana vitu vya
msingi au changamoto ni jambo ambalo huimarisha sana mahusiano na kuthaminiana
sana.
150. Kila siku
jisurutishe kufanya vitu vinavyoonekana ni vigumu na jitahidi kufanya zaidi ya
kawaida. Katika uwanja wa mashindano washindi hujitahidi kusukuma bahasha zao
za mafanikio kuelekea kileleni kwa kila wapatapo nafasi. Fanya vitu vile
unavyoogopa kuvifanya kwamba haviwezekani na ndivyo kifo cha uoga ndani mwako
kitakavyokuja. Washindi mara zote hufanya vitu vile ambavyo watu wengi wenye
maendeleo ya chini huwa hawafurahii kufanya. Hivi ndivyo tabia na shauku
vinaimarishwa ndani ya mtu. Shughulika na udhaifu ulio ndani mwako. Anza kufanya
vile vitu ambavyo ulivitenga na kutokuvifanya. Andika vile vitu katika orodha
ambavyo umevibeza mara nyingi. Fanyisha mazoezi misuli yako ya nidhamu
utakutana na siku ambayo utajisikia kujaribu kufanya vitu vile ambavyo kwa
kawaida usingevifanya ndivyo mabadiliko yatakavyokuja kwako.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni