UTANGULIZI
Ø Upungufu wa madini joto ni tatizo kubwa linaloathiri afya na maendeleo
ya jamii ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali na uchumi.
Ø Tatizo la upungufu wa madini joto hapa Tanzania ni la tatu kwa ukubwa
katika matatizo ya lishe, likitanguliwa na tatizo la upungufu wa nishati na
utomwili na upungufu wa wekundu wa damu.
Ø Ukubwa wa tatizo la upungufu wa madini joto huanishwa kwa kupima uvimbe
wa tezi la shingo na matumizi ya chumvi yenye madini joto.
Ø Tafiti za 2004 zinaonyesha kuwa uvimbe wa tezi la shingo ni 7% huku,
Ø Utafiti wa 2010 ukionyesha kuwa kaya zinazotumia chumvi yenye madini
joto ni 82% na;
Ø Asilimia 47 ya kaya zinatumia chumvi yenye kiwango cha madini joto ya
kutosha.
Mada ya 1:
TATIZO LA UPUNGUFU WA MADINI JOTO MWILINI
TATIZO LA UPUNGUFU WA MADINI JOTO MWILINI
MALENGO YA ELIMU YA MADINI
JOTO
Mwishoni msomaji
utaweza:
Ø Kufahamu maana na umuhimu wa madini joto
Ø Kuelezea ukubwa wa tatizo hapa Tanzania na kutaja maeneo yanayoathiriwa
zaidi na upungufu wa madini joto
Ø Kuelezea sababu zinazochangia upungufu wa madini joto mwilini
Ø Kuelezea madhara na athari zitokanazo na upungufu wa madini joto
mwilini
Umuhimu wa madini joto
Ø Madini joto ni moja ya virutubishi muhimu kwa ukuaji mzuri wa akili na
mwili.
Ø Madini hayo hupatikana ardhini.
Ø Binadamu anahitaji madini joto kiasi cha kijiko kimoja tu cha chai kwa
maisha yake yote.
Ø Kwa wastani mtu mzima anahitaji kiasi cha mikrogramu 100-150 ya chumvi yenye madini joto kila siku.
Ø Mahitaji kwa akina mama wajawazito ni makubwa zaidi (mikrogramu
175).
Ø Ingawa kiasi hicho cha matumizi ya madini joto ni kidogo sana lakini
umuhimu wake mwilini ni mkubwa sana.
Ø Ili kukidhi mahitaji ya mwili,
binadamu anatakiwa apate madini joto kila siku. Kwa maana hiyo madini joto
lazima yawe sehemu ya chakula chake.
Ø Madini joto hutumika katika kutengeneza vichocheo au homoni za tezi la
shingo “thyroid hormones”.
Ø Homoni hizi husaidia katika ukuaji bora wa mwili na ubongo pamoja na
mfumo mzima wa fahamu.
Ø Iwapo madini joto yatakosekana, kichocheo hiki kitashindwa kutengenezwa
na hatimaye mtu atapata madhara.
Ø
Madini joto pia ni muhimu wakati wa
ujauzito kwa ajili ya ukuaji wa mtoto aliye tumboni, kuzuia ulemavu wa akili na
mwili na ukuaji mzuri wa mtoto baada ya kuzaliwa.
Ø
Madini joto huhitajika kwa wingi wakati wa
mabadiliko ya kimwili kama vile wakati wa kuvunja ungo au kubarehe.
Ø
Madini
ni muhimu katika kuongeza uwezo
wa kuelewa,kutenda na kufundishika.
Ø
Kwa watu wazima madini joto huongeza
uchangamfu wa mwili hivyo kuongeza uwezo wa kufanya kazi na kuongeza tija.
UKUBWA
WA TATIZO
Ø Tanzania ni kati ya nchi ambazo zinaathirika kwa kiwango kikubwa na
tatizo la upungufu wa madini joto mwilini.
Ø Tatizo hili linawaathiri watu wengi na hasa wanaoishi sehemu za
miinuko za nyanda za juu kusini, yaani
mikoa ya Njombe, Mbeya, Iringa na Rukwa.
Ø Mikoa mingine inayoathirika ni
Ruvuma, Kigoma, Kagera na baadhi ya sehemu za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,
Dodoma na Morogoro.
Ø Matumizi ya chumvi yenye madini joto katika kaya yamekuwa yakiongezeka
hadi kufikia 83% na yanatarajiwa kupunguza kwa kiasi kikubwa au kutokemeza kabisa tatizo la upungufu wa madini joto
mwilini.
SABABU ZA UPUNGUFU WA
MADINI JOTO MWILINI
Ø Madini joto hupatikana ardhini. Binadamu huyapata madini hayo kwa kula
vyakula vinavyopatikana kwenye ardhi hiyo.
Ø Kiasi cha madini joto katika chakula hutegemea wingi wa madini hayo
ardhini.
Ø Maeneo ya miinuko na milima huwa na kiasi kidogo cha madini hayo.
Ø Hii ni kwa sababu katika maeneo hayo madini joto yanakuwa yamepotea
kutokana na kuchukuliwa na maji (mvua, miti, chemchem, mafuriko) na kuelekezwa
mabondeni na baharini/ziwani.
Ø Kwa sababu hii vyakula vya baharini au vinavyopatikana mabondeni huwa
na madini joto kwa kiasi kikubwa sana.
Ø Wakati huohuo watu waishio maeneo yenye miinuko na milima hupata upungufu wa madini joto.
ATHARI ZITOKANAZO NA
UPUNGUFU WA MADINI JOTO MWILINI
Ø Mtu anapokosa madini joto ya kutosha mwilini hushindwa kutengeneza
homoni za tezi la shingo, upungufu huu
una athari kubwa za kiafya.
Ø Mifumo ya mwili iliyo mingi huathirika kwa viwango mbalimbali lakini
ubongo wa mtoto aliye tumboni huathirika zaidi.
WAKATI
WA UJAUZITO:
- Mimba kuharibika
- Mtoto kuzaliwa akiwa mfu (amekufa)
- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake (njiti)
- Mtoto kuzaliwa na uzito pungufu
- Mtoto kufa akiwa mchanga
- Mtoto kuzaliwa na ulemavu wa viungo
- Mtoto kuzaliwa akiwa kiziwi na kuishia kuwa bubu
- Kudumaa kwa mwili na utaahira
Cretinism
Ø Hii ni
hali inayojitokeza panapokuwa na upungufu wa madini joto uliokithiri ambao
hutokea tangu mtoto akiwa tumboni kama inavyoonyesha katika kielelezo cha picha
ya kwanza.
Ø Mara
nyingi mtoto huzaliwa na mtindio wa ubongo.
Pamoja na hayo mtoto huweza kuwa kiziwi au bubu kudumaa kwa akili na mwili.
WAKATI WA UTOTO
Ø Kuchelewa katika hatua za
ukuaji na maendeleo
Ø Ugumu katika kuelewa,
kutenda na kufundishika
Ø Kuchelewa kubarehe au
kuvunja ungo
Wakati wa Utu Uzima
Ø
Endapo patakuwa na upungufu au kukosekana kwa madini
joto, tezi hilo litachochewa kufanya kazi ya ziada ya kutengeneza kichocheo
hicho hatimaye kuongezeka ukubwa.
Ø
Kuvimba kwa tezi la shingo " Goitre “
Ø
Uvimbe wa tezi la shingo unaweza kuwa mkubwa kiasi cha
kubana njia ya chakula na kufanya mtu kupaliwa au kumeza chakula kwa shida.
Uvimbe pia unaweza kubana njia ya hewa na kusababisha kupumua kwa shida.
Ø
Kupungua kwa kasi ya kufikiri na kutenda(kufanya)
kazi
Ø
Kutostahimili
hali ya baridi
Ø
Kuwa
na hali ya ulegevu, kukosa uchangamfu
Ø
Hali
ya kufunga choo
KIJAMII
NA KIUCHUMI
Ø Jamii hutumia muda mwingi
na rasilimali katika kuwatunza waathirika wa upungufu wa madini joto.
Ø Mifugo pia huathirika na upungufu
wa madini joto, kama walivyo binadamu;
Ø kuharibu mimba, kudumaa na
kuongezeka kwa vifo. Yote hayo husababisha hasara za kiuchumi.
Ø Madini joto ni moja ya
virutubishi muhimu kwa ukuaji mzuri wa akili na mwili .
Ø Madini haya hupatikana ardhini.
Ø Mahitaji ya madini joto kwa
binadamu ni kiasi cha ug. 100-150 kwa siku.
Ø Mvua za mara kwa mara
huyachukua madini joto kutoka ardhini katika sehemu za miinuko kwenda
mabondeni, baharini /ziwani na kusababisha vyakula vinavyolimwa katika maeneo
hayo kuwa na upungufu wa madini joto
Ø Madhara na athari za
upungufu wa madini joto ni pamoja na kuvimba kwa tezi la shingo, udumavu wa
akili na mwili, matatizo ya uzazi, vifo vya watoto na kushuka kwa hali ya
uchumi na maisha.
Mada
ya 2
Mikakati ya Kukabiliana na Upungufu wa Madini Joto
Mikakati ya Kukabiliana na Upungufu wa Madini Joto
Ø Kumekuwa na mikakati kadhaa
ya kukabiliana na tatizo hili nchini ambayo imesaidia sana kupunguza tatizo la
upungufu wa madini joto katika maeneo
yanayoathiriwa sana na tatizo hili.
Ø Hapa nchini baadhi ya mbinu
zilizotumika ni pamoja na Utoaji wa madini joto ya nyongeza, uwekaji wa madini
joto kwenye chumvi, uhamasishaji wa matumizi wa chumvi yenye madini joto na
ufuatiliaji wake katika jamii.
Utoaji wa Madini joto ya nyongeza km:
- Lugol’s iodine (matone ya vitamin A)
- Dawa ya sindano yenye madini joto
- Vidonge vyenye madini joto
Uchanganyaji wa Madini joto kwenye
chumvi
o Uagizaji wa mashine na
vifaa vya kuchanganya chumvi na madini joto km; madini joto, iodine test kits
na vifungashio
o
Mafunzo
kuhusu matatizo yatokanayo na upungufu wa madini joto pamoja na uzalishaji wa
chumvi bora na yenye madini joto kwa Maafisa Afya na wazalishaji chumvi.
Elimu
kwa umma kwa kutumia mkakati wa mawasiliano (Mikutano ya hadhara)
- Uhamasishaji wa viongozi katika ngazi mbalimbali zikiwemo halmashauri zote.
- Utumiaji wa vyombo vya habari km TV, Radio, Magazeti nk.
- Uhamasishaji wa wazalishaji chumvi kujiunga ktk vikundi
- Kuanzishwa kwa Chama cha Wazalishaji Chumvi Tz na kuwepo kanda tano, Chama kina majukumu yafuatayo:
- Kuwaunganisha wazalishaji chumvi na wadau wengine
- Kufuatilia uzalishaji wa chumvi yenye madini joto
- Kuhakikisha upatikanaji wa madini joto na vifaa vingine
- Kuhamasisha wazalishaji chumvi kuhusu uzarishaji wa chumvi yenye madini joto
- Kuwepo kwa Kamati Ya Kitaifa inayoratibu mpango wa kudhibiti upungufu wa madini joto.
- Kuanzishwa kwa sheria ya chumvi
Ufuatiliaji
na tathmini:
- Katika ngazi ya jamii
- Kwenye mashamba ya chumvi, maduka na viwandani
- Utekelezaji wa sheria ya chumvi
MAFANIKIO
- Ongezeko la kaya zinazotumia chumvi yenye madini joto kutoka 0% (1980) hadi 82% (2010)
- Idadi kaya zinazotumia chumvi yenye kiwango cha madini joto ya kutosha zimeongezeka kutoka 43% (2004) hadi 47% (2012)
- Uvimbe wa tezi la shingo umepungua kutoka 25% (1980) hadi 7% (2004)
- Uwepo wa maabara 18 za kufuatilia ubora wa chumvi yenye madini joto. Kati ya hizo; 6 ni za wazalishaji chumvi (Dsm, Tanga, Bagamoyo,Kilwa, Lindi, Mtwara),12 zipo ktk wilaya zinazozalisha chumvi kwa wingi (Ruvuma, Mbeya, Kyela, Iringa, Dodoma, Morogoro, Arusha, Mwanza, Tabora, Mtwara, Njombe na Tanga)
MIKAKATI ENDELEVU:
- Kuhakikisha upatikanaji wa madini joto kwa wazalishaji chumvi
- Kuimarisha ufuatiliaji wa chumvi yenye madini joto;
- Kuimarisha utekelezaji wa sheria ya chumvi;
- Kuhamasisha umma kuhusu matatizo yatokanayo na upungufu wa madini joto mwilini
- Kuwawezesha wazalishaji wadogo wa chumvi ktk yafuatayo:
Ø Upatikanaji wa madini joto
wakati wote.
Ø Kuwapatia mafunzo ya
uzalishaji bora wa chumvi yenye madini joto.
Ø Kuhakikisha upatikanaji
wa test kits na vifaa vingine muhimu km
vile vya maabara na pampu.
Ø Kuoanisha ufuatilaji wa
chumvi yenye madini joto na programu nyingine:
Ø Juhudi zimefanyika katika
kuingiza masuala ya kudhibiti upungufu wa madini joto na ufuatiliaji wa chumvi
yenye madini joto katika mipango ya halmashauri badala ya kutegemea wafadhili.
Kuhamasisha
viongozi:
Ø Katika ngazi za maamuzi juu
ya matatizo ya upungufu wa madini joto mwilini na uzalishaji wa chumvi yenye
madini joto.
Ø Katika ngazi za halmashauri
ili waweze kuingiza masuala ya kudhibiti upungufu wa madini joto na ufuatiliaji
wa chumvi yenye madini joto katika mipango ya halmashauri
CHANGAMOTO:
Ø Uwepo wa wazalishaji wadogo
wengi wa chumvi waliotawanyika ktk maeneo tofauti na maeneo mengine si rahisi
kufikika
Ø Kutokuwepo na upatikanaji
endelevu wa madini joto
Ø Mapungufu katika mfumo wa
usambazaji wa madini joto
Ø Gharama kubwa ya madini
joto (kg 1 = Sh. 60,000/=)
Ø Usimamizi hafifu wa
utekelezaji wa sheria ya chumvi
Ø Wazalishaji kutofuata
vigezo vya uzalishaji bora wa chumvi yenye madini joto (Viwango vya madini
joto, usafi, uhifadhi n.k)
Ø Uelewa mdogo kuhusu:
Ø Uchanganyaji wa madini joto
kwenye chumvi kwa wazalishaji,
Ø Umuhimu wa matumizi ya
chumvi yenye madini joto kwa jamii
MATARAJIO:
- Kuendelea kuhamasisha viongozi, wazalishaji chumvi na jamii
- Kuimarisha ufuatiliaji wa chumvi yenye madini joto na utekelezaji wa sheria ya chumvi yenye madini joto
- Kutafuta njia ya upatikanaji endelevu na usambazi mzuri wa madini joto
- Kufanya tafiti kwa makundi yenye mahitaji maalum mf. Watoto wadogo, wanawake wajawazito na wazee.
IMEANDALIWA
NA;
Beatrice Bethod-Afisa Lishe-Ludewa
Simu Na-0752472813
Email- beatricebethod@gmail.com
Beatrice Bethod-Afisa Lishe-Ludewa
Simu Na-0752472813
Email- beatricebethod@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni