141. Watu
wengine huviona vitu kama vilivyo na kusema “kwanini?” Ninaota ndoto ya vitu
ambavyo sijawahi kuviona na kusema “kwanini iko hivi na si vinginevyo?” Hii ni nukuu
toka George Bernard Shaw.
142. Tumia mbinu
zifuatazo katika kuongeza ubora wa akili yako katika kutafakari:
1. Jizoeshe kutafakari kila
siku mahali palepale na muda uleule ili ufahamu wako uwe tulivu.
2. Alfajiri ni muda mzuri na
tulivu sana kwa kutafakari. Hili litakuongezea amani katika kuyaendea mafanikio
yako.
3. Kabla ya kuanza amru
ufahamu wako utulie kwa kutumia hisia “nitakuwa makini na mtulivu kuanzia sasa”.
4. Kama mawazo yanakujia
usilazimishe kuyaondoa bali yaache yakutengenezee njia nzuri ya
mafanikio.Tambua kwamba ufahamu wako ni kama
ziwa lisilo hata na mawimbi.
5. Kaa kwa dakika kumi kwa
mara ya kwanza baadae ongeza muda kila baada ya dakika kumi. Baada ya mwezi
mmoja au miwili hautakuwa unaingiliwa na mawazo yanayo changanya ufahamu wako
na utahisi utulivu wa hali ya juu ambao hujawahi kutana nao.
143. Weka urafiki
wa haliya juu na watu mahusiano haya ni muhimu na itakusaidia kuwa na afya
nzuri na maisha yenye mafanikio.Tafuta muda mchache kila siku wa kuwasiliana na
watu ambao hujawasiliana nao kwa muda mrefu. Onesha upo pamoja nao na angalia
matokeo baada ya kuwasiliana nao. Jenga tabia ya kuwa na urafiki mzuri na wa muda
mrefu na watu. Pia weka kipaumbele kupata marafiki wapya bila kujali utakuwa
nao kwa muda gani. Hii ni moja ya njia ya mtu kufurahi ambayo watu wengi
huikosa.
144. Ni
vizuri kuupata muziki laini baada ya shughuli zako nzito ili kukuburudisha na
hakika muziki wa namna hii huiburudisha roho yako.
145. Ishushe
hamu uliyonayo kwa kunywa maji mengi. Shusha kiu yako kwa kunywa maji tena na
tena ukifikisha glasi kumi kwa siku itakufaa sana! Inauweka vizuri mwili wako. Pia
jizoeshe kunywa supu ikiwa na mchanganyiko na vyakula vyenye wanga ili
kukuondolea njaa na kuufanya mwili wako ujisikie vizuri. Upo jinsi ulivyo
kwasababu ya vyakula unavyokula na hakikisha wakati wote mlo wako unakuongezea
nguvu na kuimarisha akili yako.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni