136. Furahi
kazini na ujulikane kwa wengine kama mtu wa kufanikiwa.
137. Wazo
huleta taswira katika akili. Taswira katika akili huzalisha mazoea ya akili
mwishowe katika kupambanua aina ya mambo. Tawala mawazo yako, utawale
kumbukumbu zako na utawale maisha yako; ukitawala maisha yako utatawala na
mafanikio yako.
138. Tambua
nguvu kubwa ya mawazo tofauti. Hii ni kanuni nyepesi inayohusisha badiliko la
mtizamo chanya kuwa mtizamo hasi na vizuizi vinavyoingia akilini mwako na
kupunguza malengo yako wakati wote. Mfano; Jumapili jioni unaweza kufikiria “natamani
nisingeenda kazini kesho baada ya mapumziko na raha niliyoipata mwishoni mwa
wiki”.Ghafla utaona yanakuja mawazo yanayo kabili nia hiyo hata kabla haijaanza
kujijenga. Mfano mwingine “siwezi kusubiri kwenda kazini kutokana na shughuli
zinazosisimua zinazoendelea na hisia ya ajabu kwa matokeo na changamoto
nilizopata mwishoni mwa wiki”. Alafu fikiri bahati uliyonayo kwamba una kazi na
jinsi unavyoweza kufanya kwa jitihada zako hata kuwa na matokeo makubwa.
Fikiria na orodhesha vitu vinavyoweza kukufanya ufanye vizuri vilivyomo ndani
mwako na rudia kwa kufanya hivyo tena na tena. Baada ya muda mfupi utaona vitu
vile vya kukuvunja moyo na kukukatisha tamaa vikitoweka kimoja baada ya kingine
na kukufanya ufanye vizuri zaidi na kuifurahia wiki yako kwa ari zaidi.
139. Jizoeshe
kujipima wewe mwenyewe. Ben Franklin aliitaja hii kama mbinu muhimu zaidi
katika mafanikio ya mtu binafsi. Tumia dakika kumi kila siku kujichunguza wewe
mwenyewe binafsi. Fikiri juu ya vitu vizuri ulivyovifanya katika siku yako na
tabia mbaya inayoweza kukurudisha nyuma ambayo unalazimika kuibadili ili
uongezeke na kustawi sana! Watu waliofanikiwa ni wale wanaotafakari mambo zaidi
ya wengine. Tendo la kujiakisi litakuondolea sifa mbaya na kuunoa ubongo wako. Baada
ya muda utashangaa makosa unayofanya ni machache sana na ujasiri juu yako
utaongezeka na kukupeleka ngazi nyingine ya juu zaidi.
140. Hadhari nzuri na ya kufaa imejengwa ndani ya
akili yako. Kama huamini jaribu yafuatayo:
1. Keti katika kiti cha
kawaida kwa wastani wa dakika 10 kabla ya kwenda kulala.
2. Funga macho yako alafu
taratibu elekeza mikono yako magotini.
3. Pumua kwa nguvu kwa dakika
chache (vuta hewa kwa sekunde tano, kisha tulia kwa sekunde kumi na pumua
kikamilifu)
4. Rudia yafuatayo mwenyewe
angalau mara ishirini: “Nitaamka nitakapojisikia vizuri, mchangamfu na mwenye
shauku.” Maneno hayo lazima yatamkwe kwa hisia na shauku. Alafu baada ya
sekunde chache hebu tafakari wewe mwenyewe pale unapoamka kwa wakati unaoutaka
na fikiri utajisikiaje!!?. Utajikuta unaamka muda uutakao bila hata ya mazoezi.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni