Jumapili, 6 Novemba 2016

NA.131 - NA.135: ACHA SAA YAKO NYUMBANI!



131. Kuza akili ya mshangao juu ya dunia. Uwe mtafiti wa mambo. Tafuta furaha katika vitu walivyonavyo wengine ambavyo wewe kwasasa huna. Jitahidi kusoma vitabu bora kabisa ambavyo wazazi wako walivipenda sana. Panga kutoka nje ya mji wako kwa matembezi ya kawaida wiki linalofuatia na tembelea maeneo yenye utulivu, maeneo yenye uasili kwa siku chache tu. Jaribu kujirudisha nyuma kidogo na uangalie yale yaliyopita ukitafakari ya mwilini na ya kiroho pia. Kufanya vyote hivyo kuna maana sana katika kuyaboresha maisha yako.
132. Watumie jamaa au marafiki zako kadi za kumbukumbu ya kuzaliwa na andika maneno machache mara kwa mara kuonesha kwamba unawajali na pia unathamini mahusiano yako na wao. Sote tuna shughuli nyingi lakini kutumia dakika tano katika wiki kuwakumbuka marafiki na jamaa zako, kwa mwaka mzima utakuwa umetuma kadi 52. Huu ni uwekezaji mdogo kama dhamana ya gawio ambalo litakuja kwako au litakufuata.
133. Kumbuka na tumia jina la mtu unapoongea na watu. Jina la mtu linaleta upekee na kuongeza uzito kwake.
134. Kutoka katika mazoea na kufanya jambo ambalo si la mara kwa mara kama kuangalia anga la bluu, kutembelea maeneo yenye uasili kunakuongezea nguvu zaidi na kuchangamsha akili yako. Tembelea misitu ya asili na kaa kidogo ukipata upepo tulivu au waweza kodi mtumbwi na kutalii kidogo maeneo ya bahari au maziwa. Kufanya hivyo kutakushangaza baada ya kurudi. Kwani utajiona kama mpya kabisa.
135. Kila baada ya wiki kadhaa acha saa yako nyumbani. Katika jamii tumekuja kujikuta tunafungwa na saa zetu kiasi cha kuongozwa na saa kwa kila jambo kama msimamizi wa majukumu yetu. Nenda siku nzima ukifanya yale uliyokusudia kuyafanya kwa usahihi hata kama ingekuchukua muda mrefu sana. Tumia muda na watu mashuhuri bila kukimbia kimbia katika miadi mingine. Okoa muda na lenga katika jambo lililo muhimu badala ya vitu vingine vya dunia ambavyo wakati mwingine vinaonekana ni vya muhimu zaidi kuliko uhalisia. Acha saa na upate muda ulio bora.

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,

\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: