Alhamisi, 3 Novemba 2016

NA.129: JENGA URAFIKI MPYA.



    Uwe ni mtu unayejituma na mwaminifu kwa wengine. Jenga urafiki mpya. Utashangaa namna watu wanavyokukumbuka kwa miaka mingi baadaye kwa vitu vidogo vidogo sana ulivyowatendea, matendo ya wema kwa wengine yatakusaidia katika maisha yako baadaye. Kila anayekuja kwako mhudumie kana kwamba ni mtu muhimu sana katika dunia yako. Kwa hakika utakutana na mafanikio makubwa sana.

Hakuna maoni: