Alhamisi, 3 Novemba 2016

NA.128: UNAPASWA KUJULIKANA KWA WENGINE.



       Unapaswa kujulikana kwa wengine kwamba wewe ni mtu unayekwenda masafa. Mtu unayefanya kazi kwa muda mrefu zaidi ya wengine. Mtu unayefanya zaidi ya kawaida na mfuatiliaji na mwenye mafanikio makubwa. Jiweke kuwa ni mtu unayewaza juu ya wengine na unayeifanya hata familia ijisikie kuwa ina mtu muhimu sana. Uwe ni mtu mwenye msimamo lakini unayeweka mizania sawa kati ya utu na weledi. Uwe ni nyota inayong`ara na kuwafanya wengine kukutazama na kupendezwa.

Hakuna maoni: