Ni muhimu
kuvunja mazoea yanayojengeka ndani mwako yanayokuletea mashaka katika mafanikio
unayotaka kuyafikia na uyafunike mashaka hayo na taswira ya jambo unalotaka
kuliendea na pia uucheke ushindani mdogo mdogo unaotokea katika safari yako ya
mafanikio. Endelea kujipa moyo juu ya ugumu unaopitia na kusema kwa
kurudiarudia kwamba hili ni jambo la muda mfupi tuu! Alafu chukua kipande cha
karatasi, andika mashaka uliyonayo ndani mwako.Ugawe muda wako kidogo
kuyafikiri hayo, yatenganishe matatizo yako na kubuni njia mbadala ya
kuyakabili. Kwa kufanya hivyo mtizamo hasi uliomo ndani mwako na nguvu ya
mazoea itapotea kabisa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni