121. "Leo
yako ni mwanafunzi wa jana." - Benjamin Franklin
122. Kama
umechagua njia mbili basi nenda na njia ile inayokupa shauku zaidi. Jiridhishe
kwa kukokotoa vihatarishi utakavyo kutana navyo katika kukupa matokeo uliyo ya
kusudia.
123. Kila
siku jitahidi kupata muda wa kujitenga na kelele, msongamano wa watu na uende
mahali penye utulivu na amani kwa nia ya kujipima au kujichunguza, usomaji wa
kuzama au mapumziko ya kawaida.
124. Angalia,
mtu yeyote aliyetembea duniani amefanikiwa! Unaweza kufanikiwa katika mtizamo
sahihi, uvumilivu na bidii ya kazi. Mawazo na akili dhaifu havinabudi
kudhibitiwa na kukomeshwa. Malengo ya mtu lazima yatulie kuuangalia mwisho wa
jambo lenyewe na hilo ndilo jambo la muhimu.
125. Jijengee
mazoea ya kujikumbusha mashairi yale mazuri. Si tu kitakuwa ni chanzo chako cha
kujiburudisha bali inakuza utendaji wa akili yako kukupeleka katika ngazi ya
juu zaidi katika kumbukumbu, kuunganisha mambo mbalimbali na wepesi wa akili.
126. Maneno
yako yawe laini na hoja zako nzito.
Kwa leo tuishie hapa na
karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni