Alhamisi, 3 Novemba 2016

NA.130: WATU MASHUHURI HUVUTA MAFANIKIO.



     Ukitafuta chochote kwa bidii ni lazima utakipata. Ukitafuta mafanikio ya tofauti na wengine kwa hakika utayapata. Watu mashuhuri huvuta mafanikio. Ni lazima uweke malengo yako unayoyatamani kuyafikia mbele ya mambo yote katika kila siku. Jikumbushe matamanio yako walao mara tano kwa siku na jipe taswira ya namna ya kuyapata. Kama lengo lako ni kuwa tajiri, pata taswira ya nyumba utakayoishi, gari utakalokuwa unaliendesha mwenyewe, namna utakavyojisikia kama tajiri na furaha ya kuyafikia malengo katika maisha yako. Rejea malengo yako tena na tena mpaka uhakikishe mashaka ya kufikia malengo yako yametoweka na kwamba utapata haja yako na hapo mwishowe itakuwa!

Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: