Jumatano, 19 Oktoba 2016
NA.91 – NA.95: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA
91. Chukua lengo moja wapo liendeleze kwa umakini, na kuonesha kipaji cha peke yake. Ubora wa namna hiyo kila mmoja wetu anaweza kuuonesha katika kutekeleza lengo kwani kila binadamu ana kitu maalum ndani mwake tofauti na mwingine lakini ni wachache wanaoweza kufanya hivyo. Raisi wa marekani aitwaye Kennedy katika ujana wake aliugua sana juu ya kitu hicho kwamba aoneshe kipaji chake katika uongozi ambacho kama kiongozi wa kisiasa kwa historia ya marekani haijawahi kutokea. Anza sehemu ndogo kabisa katika kufikia lengo hili. Jifunze namna ya kuwasilisha mada mbele ya watu wengi. Nenda kwenye mitandao na tafuta vitabu vinavyofundisha sanaa ya mazungumzo na maandalizi ya wadhifa fulani. Jifunze vitu safi vitatu na uchekeshaji na tabia mwingiliano na jamii. Utakuwa na kitu cha ajabu kitakachojengeka ndani mwako na kukufanya uwe na mtandao wa marafiki na watu wengi wa kushirikiana nao.
92. Katika somo la mazungumzo, katika misemo ya ki-china husema “mazungumzo na mtu mwenye busara mezani yana thamani kubwa kuliko kusoma vitabu kwa mwezi mzima” Tafuta watu wenye busara na jifunze kutoka kwao. Wapo wengi wenye busara na hekima ambao wanakusubiri wewe uwaendee na kuuliza nini ungependa kusikia kutoka kwao.
93. Nishani tatu za ubora zilitolewa kwa Lao-Tzu kama mtu mashuhuri. “ ya kwanza ni upole, ya pili ni uangalifu, na ya tatu unyenyekevu, ambazo zilimfanya wakati wote kuwa mbele ya wengine. Ukiwa mpole utakuwa jasiri, ukiwa mwangalifu utakuwa huru, ukijiepusha kujiweka mbele ya wengine utakuwa kiongozi wa watu.”
94. W.J. Slim alisema, “Kama akili yako ina mambo mawili ambayo yote yanaonekana kuwa sawa na unashindwa lipi ulichukue kwa wakati huo, chukua lile unaloliona vizuri bila ukakasi” hakuna mbadala katika ushawishi ingawa nafasi ya kujikwaa kidole cha mguu huongezeka kadiri unavyoendelea kutembea ni afadhali kuendelea kuliko kuacha na kungojea. Itumie nafasi, chukua tahadhari ya vihatarishi ninakuhakikishia utakutana na mafanikio zaidi ya ndoto zako.
95. Jione kwamba wewe ndiwe pekee wa kujisaidia na wakati wote wa kujiwezesha kwa kuongeza mafuta ya matumaini na ndoto zako. Vyote hivi viende pamoja kokote na wakati wote kama mikono miwili ya mwanadamu.
Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni