Jumanne, 18 Oktoba 2016

MPANGO RASMI WA BIASHARA /MRADI

Ni kwa nini watu wengi wanafanya biashara bila kuwa na mpango rasmi wa biashara au mradi!?
Ili kuendesha biashara au mradi na ufanikiwe unapaswa kuwa na mpango wa biashara au mradi rasmi, na huo mpango ndio utakuwa ramani au njia ya kuiendea hata ufikie ndoto zako. Sasa wengi kwa kutokujua wanakwepa kuandaa mpango rasmi wa biashara au mradi kwa sababu zifuatazo:-
1.Kukosa uelewa na hatua zinazohitajika kuandaa mpango wa biashara au mradi.
2.Kujizamisha kutenda biashara au mradi kuliko kutafakari au kukusanya taarifa za biashara au mradi kwenye eneo unalokusudia kufanya shughuli hiyo.
3.Udanganyifu katika moyo wa mtu kwamba mpango mkakati ni kwa taasisi kubwa na biashara kubwa kubwa zenye rasilimali za kutosha.
Ndugu yangu, hakuna namna utafikia ndoto ya mafanikio katika maisha yako kwenye biashara au mradi pasipo kufanya maandalizi ya mpango rasmi wa biashara au mradi. Na hii imepelekea wengi kuchukua mikopo mikubwa, kuanzisha biashara kwa mikopo hiyo baada ya muda mfupi wengi wamefilisika na kukata tamaa kabisa.
Unataka kuanzisha biashara au mradi kwanza andaa mpango rasmi wa biashara au mradi na ninakuhakikishia ukizingatia hili Hakika biashara yako au mradi utafanikiwa.
Endelea kujifunza na kusoma maarifa kupitia blog hii  "ujasiriamaliafya.blogspot.com"  utachipua, utakua na kustawi sana ukizingatia ushauri wetu.
Usiku Mwema!

Hakuna maoni: