Jumamosi, 22 Oktoba 2016

NA.96 – NA.100: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

96. Fikiria watu watatu ambao wanaweza kukupa msukumo, kukutia hamasa na kuwezesha malengo yako na vile unavyovitamani. Jipangie kukutana na mmoja baada ya mwingine kwa wiki kadhaa mbele yako. Sikiliza kwa shauku kutoka kwao na jaribu kupeana nao mawazo ili kutafuta njia mpya za kufanyia kazi. Jichoree ramani ya kimkakati na uchukue ushauri wao wa busara ili uufanyie kazi.
97. Ifanye kila siku kwako kama ni siku ya kuitawala kikamilifu. Wahenga walisema kwa kiingereza “it's not who you think you are that holds you back but what you think you're not."
98. Nguvu za thamani kupotezwa kwa kutumia muda kwa vitu visivyo na thamani. Nguvu zaweza kupotezwa katika kufikiri vitu visivyo na tija. Kama kutafakari kwako kungepimwa kwa kipimo cha wati 1000 kama nguvu ya akili. Muda wowote unapokaa bila kutafakari juu ya miradi yako, kukaa katika mashaka, kwa vitu vyote ambavyo ungefanya, mwishoni mwa siku unapoteza wati 100. Baada ya muda kitambo kidogo nguvu zote zimepotea. Hii ndiyo asili ya akili. Kushindwa kujitia nidhamu nguvu hupotea na mwisho wake mafanikio yako yanakuwa ya chini sana. Ukidhibiti hilo utaona mambo makubwa yakitokea kwa jitihada zako. Utajikuta unakuwa jasiri zaidi na kufanikiwa katika majukumu ambayo yalionekana kuwa magumu sana yakiwa rahisi. Katika karne ya 19 Mwanafalsafa Henri FredrickAmiel, alijumuisha kwa kusema, “kwa lengo la kutenda, hakuna kitu chenye nguvu kama kupunguza fikra ukichanganya na nguvu kutaka kwako”.
99. Imekuwa ni sahihi kusema, “ unapanda vitendo, unavuna mwenendo. Unapanda mwenendo unavuna tabia. Unapanda tabia unavuna takdiri”. Hali ya mtu ni tabia yake- jiweke katika hali ya kujitambulisha (upekee), isio na dosari na imara. Usiseme utafanya chochote labda ufanye kweli. Zungumza ukweli na pima maneno yako kwa hekima. Uwe mnyenyekevu, usiopindapinda na mwenye amani.
100. Kumbuka sheria ya asili ya kufanya kinyume: mtizamo chanya siku zote huushinda mtizamo hasi. Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,

\\ujasiriamaliafya georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: