Jumatatu, 17 Oktoba 2016

NA.87 – NA.90: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

Mpendwa msomaji mwenzangu na mfuatiliaji wa makala za ujasiriamaliafya, salaam! Tuendelee kuangalia mfululizo wa siri za mafanikio katika maisha na hapa leo tutaangalia mfululizo na.87 hadi na.90. Fuatana nami sasa;-
87. Katika kujiweka kwenye hali nzuri ya utendaji kiakili, ni lazima mwili wako uwe huru. Kwasasa katika mijadala mbalimbali imethibitika kwamba kuna ushirika mkubwa kati ya mwili na kumbukumbu ikiwa kuna usumbufu na upo huru kabisa, akili ipo vizuri na inafanya kazi yake sawasawa. Hii ndiyo maana mazoezi ya viungo ya mwili yanafaida nyingi sana. Ina ufanya mwili na akili kutulia na kufanya kazi sawasawa. Kwa kawaida mazoezi ya dakika 15 kwa siku yanatosha kabisa kukufanya uende vizuri katika kutafakari na kuendesha mambo yako ukiwa na afya njema. Mazoezi ya viungo kwa kutumia jakuzi, kuruka kamba, kuruka kichura au pushaapu kidogo kidogo ni vya muhimu sana katika kuupumzisha mwili na akili. 88. Andaa mipango yako ya fedha kwa miaka kadhaa mbele na hakikisha unaizingatia. Omba ushauri wa kitaalamu kwa mambo ya fedha kama ukiona ipo haja. Mkakati wenye nguvu katika utawala wa fedha zako ni rahisi: tenga asilimia kumi ya kila fedha unazopata kama mkakati wa muda mrefu (tenga fedha hizo kila unapozipata kabla ya kuanza matumizi yoyote). Mfano ukiweka kila mwezi shilingi 200 kwa miaka 30 katika benki inayotoa faida ya asilimia 15 kwa mwaka, mwisho wa miaka hiyo utakuwa na shilingi milioni 1.4 fedha za kitanzania. Matumizi yenye busara kwenye fedha zako ni uwekezaji bora sana. Uhakika wa kifedha unakupa uhakika wa uhuru binafsi.
89. Wasomi ni viongozi. Aliyewahi kuwa raisi wa marekani kabla ya George Bush, Mheshimiwa Bill Clinton alisoma vitabu 300 katika muda mfupi sana akiwa chuo kikuu cha Oxford. Kadhalika watu waliofanikiwa sana, husoma kwa wastani wa kitabu kimoja kwa siku. Tafuta habari na maarifa kwa nguvu zako zote. Ni kweli sasa tumeingia ulimwengu wa habari na wale wanaopenda habari na maarifa wataitumia nafasi hii kwa faida yao. Kadiri unavyopata habari na maarifa ndivyo uwoga unavyokuwa mbali nawe (“the more you know the less you fear”).
90. Jijengee tabia ya kusoma kitu unachodhani ni kizuri na cha kusaidia kuboresha kazi zako kabla ya kwenda kulala na asubuhi na mapema unapoamka. Muda mfupi utagundua faida zitokanazo na fikra hii ambayo itakusaidia katika siku nzima ya shughuli zako. Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,

\\ujasiriamaliafya georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: