Jumapili, 16 Oktoba 2016

NA.81 - NA.86: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

Mpendwa msomaji na mfuatiliaji wa makala za ujasiriamaliafya, ili kufikia mafanikio ni vitu vingi utakutana navyo ambavyo vitasimama kama kizuizi kwako katika kuyaendea mafanikio yako. Ni kwa msingi huu tuendelee kujifunza mambo ya kuyafanya ili tuweze kuifurahia safari yetu na vizuizi hivyo visiturudishe nyuma au visitukatishe tamaa;
81. Mwili ulio na afya njema huwa na uwezo wa kutafakari kwema. Jenga tabia ya kufanya mazoezi mbalimbali ambayo yataufanya mwili wako uwe vizuri na kupunguza msongo wa mawazo. Mazoezi kama kuruka kamba, push up, na karate kidogo, huufanya mwili wako kukaa vizuri wakati wote. Zaidi sana kwa wale wanaopenda kuogelea hapo napo mwili unapata raha na hivyo kufanya akili yako kupumzika.
82. Watu wengi wanaofanya vizuri leo wana uhakika kuhusu kesho yao. Maisha ya kesho hayawezi kuwa bora ikiwa hujafanya bidii kuutumia muda wako vizuri leo. Watu wengi huwaza kwamba anaweza kuja kufanya vizuri akifikia miaka 60 au zaidi. Ndugu yangu usidanganyike unavyofanya sasa kesho utakuwa unapokea majibu tuu ya jinsi ulivyoutumia muda wako jana.
83. Matumizi mazuri ya muda ni kufanya kile ulichopanga kufanya kwa wakati huo. Jitahidi kukumbuka kikamilifu ni nini ulipanga kukifanya sasa. Na ndivyo utakavyofikia malengo yako yote na utakuwa na muda zaidi kwa vitu bora zaidi. Ingawa ni ngumu kunyumbuka (kama kamba ya upinde ikikazwa sana basi upinde utavunjika ghafla). Kufuata ratiba yako uliyopanga hakuhitaji kitu zaidi ya nidhamu yako mwenyewe.
84. Mbinu ya kuangalia vizuri: kama una mashaka kuhusu kitu fulani, andika kwenye karatasi mashaka yote unayoyaona. Kisha chukua kiberiti na uwashe karatasi hiyo, kasha angalia mashaka yako jinsi yanavyoteketea kwa moto. Bruce Lee, mwana Sanaa wa medani za kivita alitumia akili hii mara kwa mara.
85. Yatenge mashaka yako katika makundi. Tenga muda kiasi kwaajili ya kutafakari matatizo, weka mikakati mizuri jinsi ya kuyashughulikia na mbinu mbadala za kutatua matatizo hayo. Hili likisha fanyika jiweke katika hali ya ustahimilivu na ushupavu kwamba sasa matatizo hayo hayawezi kurudi tena. Akili ya mwanadamu imeumbwa kwa namna ya ajabu sana! Kitu unachotamani kukisahau utaona kinakuja tena na tena, lakini kile unachohitaji kukumbuka utaona wakati unakihitaji hakipo tena. Lakini akili inatabia tena kama ya misuli kadili unavyoinyoosha ndivyo inavyozidi kujikaza. Ifanye akili yako kama mtumishi wako. Lisha chakula chenye virutubisho na habari nzuri nzuri. Itakusaidia vyema na utafanya muujiza ukiamini katika hilo.
86. Watendaji mashuhuri ni watu waliohuru kimwili lakini akili yenye mambo mengi sana. Kwa leo tuishie hapa na karibu tena,

\\ujasiriamaliafya georgemtega@gmail.com; Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: