- Orodhesha mambo yote ambayo unajitambua kama ni udhaifu kwako. Kwa hakika watu wenye kujiamini na wanaopenda kujielimisha huandika udhaifu wao na kuweka mikakati ya namna ya kuondoa udhaifu huo. Hapa kanuni ya kujitambua ndiyo inayotawala! Fahamu hata watu maarufu na hodari sana duniani wana udhaifu pia! Wengine ni hodari zaidi katika kujificha madhaifu yao kiasi kwa mtu hata aliye karibu naye sana si rahisi kufahamu. Kwa upande mwingine tena tambua mambo mazuri uliyo nayo na jitahidi kujiimarisha na kujiboresha zaidi juu ya mambo hayo.
- Kamwe usiwe mtu wa kulaumu! Utambulike kuwa ni mtu mwenye mtizamo chanya, bidii, nguvu na mwenye shauku kubwa ya kupata mambo fulani fulani mazuri. Mtu mlalamishi ni mtu aliye na mashaka wakati wote na kila jambo analoliona huliona katika mtizamo hasi, huogofya watu, na utaona mafanikio yake ni kwa sehemu ndogo sana. Katika saikolojia tunasema ili kitu kikamilike hupitia sehemu mbili; kwanza kinaumbika katika mawazo na pili kinakuja kuwa halisi. Lenga katika eneo lile linalokuleta kuwa na mtizamo chanya, jiamini katika kile unachokusudia kukitekeleza na kwamba hakuna chochote cha kukukwamisha katika utekelezaji wako. Pata taswira ya kitu hicho unachokihitaji na kwa ujasiri jiamini kwamba unakwenda kukipata. Ni hakika ndoto hiyo itakuja kuwa dhahiri!
- Usiangalie udhaifu wa marafiki zako. Kwani kila ukitaka kujua udhaifu kwa rafiki zako ni lazima utaupata. Uwe mkomavu vya kutosha kupotezea madhaifu au vitu vilivyo wafanya wengine kushindwa, lakini angalia vitu vizuri ambavyo kila binadamu anavyo. Tunaweza kujifunya toka kwa kila mtu. Kila binadamu anayo habari ambayo yaweza kuwa sehemu ya mafunzo yetu. Fungua ufahamu wako katika eneo hili na hakika utajifunza mengi naya kushangaza. Marafiki ni watu muhimu kwa furaha yetu, zaidi wale tunaobadilishana uzoefu na kucheka pamoja nao. Jitahidi kuwapata marafiki, na mahusiano imara na yenye nguvu. Waite marafiki zako wanunulie kitu unachoamini chaweza kuwapa furaha kama vitabu vidogo au chochote unachodhani ukiwapa kitawafanya wafurahi. Kama ilivyo kanuni ya shamba “ apandacho mtu ndicho atakacho vuna” itumie hii kuwapata marafiki na kumbuka ukitaka kuwa na marafiki wakubwa ni lazima kwanza uwe peke yako.
Kwa
leo naishia hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Endelea
kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni