Jumatano, 12 Oktoba 2016

NA.71 - NA.72: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.

71. Uwe na busara, huruma na heshima kwa wengine. Lakini uwe mwerevu wa kujua ni wakati gani unapaswa kuwa jasiri na shupavu. Hii ni alama nzuri ya kukutambulisha tabia yako na hakika utajipatia heshima. Ni jambo zuri kusoma vitabu mbalimbali kwa hali ya kupenda na kuimarisha mahusiano kwa kuwasikiliza wengine na kuonesha kuthamini michango yao. Hata hivyo ni muhimu kila mmoja kufahamu kuwa maneno ya hekima na uerevu ni maarifa ya kulea na kuyatunza. Maarifa ya saikolojia ya binadamu yanakuwezesha kuwasoma na kuwatambua watu. Usichukuliwe na siasa na uwe makini na mambo ya siasa katika eneo lako. Unapaswa kuwa juu ya siasa zinazoendelea na jitahidi kujua kila kinachoendelea nyuma ya siasa hizo. Kiongozi yeyote mashuhuri ndivyo anavyoishi hata kufanikiwa kwake. 72. Tengeneza taswira yako kuwa wewe ni maarufu sana, imara, hodari, mwenye nidhamu kubwa, mpole na unayeenda kwa adabu. Tafuta eneo la ulinganifu juu ya hali yako ya ndani na taswira uliyonayo juu yako. Jenga hisia ya siri juu yako kuwa ni hakika una busara bila kujionesha. Usimwambie mtu yeyote kuhusiana na jinsi ulivyo, mipango yako na hamu yako. Watu waliofanikiwa katika dunia ya leo hufikiri mara mbili kabla hawajasema kwani neno likishasemwa huwezi kulirudisha ndani tena. Onesha hali ya kuwa mambo ni rahisi na yanawezekana na hapo watu utasikia wanasema umejaliwa. Zungumza vitu vizuri tu juu yao, kwa hakika watu watakufuata na kamwe usizungumze mabaya ya wengine kwani kwa kufanya hivyo watu watafahamu kuwa hata wao wakiwa mbali na wewe utazungumza mabaya juu yao. Ijenge tabia yako na kuiishi kuwa msingi wa maisha yako. Kwa leo tuishie hapa na karibu tena, \\ujasiriamaliafya georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: