Jumamosi, 8 Oktoba 2016

NA.64 - NA.67: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.



  1. Wakati fulani unaweza kufanya jambo ambalo laweza kuonekana ni kama la kitoto au kituko kulingana na hadhi yako. Ni vizuri kuwa na mpangilio kwa kila mwezi wa kufanya mazoezi kama kupanda mlima, au kushiriki uvuvi katika maji ya kina kirefu kwa wale waishio mwambao mwa maziwa au bahari. Hii itakuweka kwenye taswira kwamba upo karibu na wote unaoshirikiana nao katika biashara au shughuli zako pale unaposhirikiana nao kwa vitendo. Na hili litakufanya ujisikie mwenye nguvu na kijana zaidi.
  2. Muda mwingine jihudhurishe au tembelea mazingira yenye uasili. Uasili wa mazingira huifanya akili yako kupumzika na kupata vitu vipya vitakavyo kufanya ukuze kazi zako au biashara zako. Watu maarufu wanafahamu hivyo kwa miaka mingi sasa umuhimu wa kutembelea mazingira yenye uasili. Tembelea ndani ya msitu au hifadhi ya misitu iliyokaribu yako. Na kama kuna kambi hata kulala hukohuko na kwa kufanya hivyo itaifanya akili yako kupata afya. Wengine hutengeneza bustani katika maeneo wanayoishi hata kama ni katikati ya mji mkubwa, mahali hapo pa bustani nzuri utakapotengeneza ndipo patakuwa badala ya kwenda kwenye maeneo ya uasili. Kutumia muda wako kidogo kwenye maeneo yenye uasili inakufanya ujisikie shwari zaidi.
  3. Tujikumbushe maneno ya hekima yanayosema “mens sana in corpora sano” yakimaanisha “akili timamu hukaa kwenye mwili wenye afya njema”. Kamwe usiudharau mwili wako ambao ndio unabeba akili yako iliyo timamu. Mwili ni kama hekalu, weka mafuta ya kuuendesha mwili wako yaliyo salama, fanya mazoezi kila siku, na uujali kama ni kitu cha thamani kuu!
  4. Tafuta mshauri ambaye ataangalia mwenendo wako na kukushauri ipasavyo. Matatizo yeyote katika dunia tunayokutana nayo si kitu kigeni wapo ambao tayari walisha yapitia na wakatafuta mbinu za kukabiliana nayo, hivyo basi uzoefu wa watu wengine unaweza kukusaidia kufanya vizuri zaidi. Tafuta mtu mwenye uzoefu na anayeweza kukutia moyo kusonga mbele. Ni lazima uwe mwenye kupenda kujua zaidi toka kwa mshauri wako na utajifunza mengi zaidi. Watu wengi wanapenda kuheshimiwa na kuthaminiwa, hivyo basi ukilitambua hilo utapata watu wengi wenye utayari wa kukusaidia hata kama mwingine anaonekana yupo na majukumu mengi sana akitambua unahitaji msaada wake wa kiutaalamu atakusaidia bila shaka.
Kwa leo naishia hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: