- Uwe hodari kiasi cha kutokuruhusu kumbukumbu zako kuvurugwa au kuingiliwa na chochote. Bondia hodari kwanza alikuwa hana furaha, na alipoulizwa ni kwanini yupo vile; alijibu “nimeamua mwenyewe kujiweka katika mtizamo hasi”. Dhibiti tama yako na kusimama katika lengo lako, ni rahisi kufanya mazoezi.Ni kweli huwezi kupata raha ikiwa una mtizamo hasi.
- Kulala usingizi kama mtoto mdogo ni jambo jema sana na ili ulale usingizi wa namna hiyo; kula mapema, masaa matatu kabla ya kulala. Hilo litaruhusu umeng`enywaji mzuri wa chakula tumboni mwako. Mazoezi ya mara kwa mara ya mwili wako yanakufanya upate usingizi kama wa mtoto, na usiendelee na kazi kitandani mfano jambo la kufadhaisha usiruhusu kwenda nalo kitandani. Mwisho Leonardo da Vinci alisema, “matumizi mazuri ya siku yako, hukuletea usingizi wa furaha”.
- Uwe makini na sifa uliyonayo katika jamii. Kama ni njema itakupandisha juu zaidi. Lakini ikiharibiwa itakuwa ni vigumu kuirejesha. Wakati wote angalia msingi wa jambo lenyewe. Usitamke jambo lolote ambalo. usingependa kulitamka. Wakati wote furahi lakini endesha mambo yako kwa akili ya kawaida na busara ili kuitunza haiba yako.
Kwa
leo naishia hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni