Jumatano, 5 Oktoba 2016

NA.56 - NA.60: MFULULIZO WA SIRI ZA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.


  1. Katika kuimarisha mahusiano ya kibiashara na wateja wako jenga mazoea ya kuwapelekea ujumbe wa kuandikwa kwa mkono. Jenga mfumo wa kukukumbusha ili kuwatumia kitu cha thamani angalau mara moja kila miezi minne, hii itasaidia kuimarisha mahusiano yako. Watumie kadi za salaam na kadi hizo ziandike kwa mkono wako usihofie rasilimali muda au rasilimali fedha utakayoitumia. Huo utakuwa ni uwekezaji wa kipekee wa muda wako. Au unaweza kuwatumia makala mpya kwenye anuani zao zitakazowahamasisha katika shughuli zao na kuwatakia heri na kwamba unathamini mahusiano yako na wao. Kujenga mahusiano mazuri kiwe ni kitu cha wakati wote bila kujali wewe ni Mtendaji Mkuu, Mwanafunzi, Mfanyabiashara au Mzazi.
  2. Vitu viwili vya msingi wa furaha , maisha ya furaha ni urari na kiasi. Ni lazima uhakikishe unaishi kwa kiasi katika kila unalo lifanya bila kupita kiasi au kuzidisha.
  3. Inashauriwa kunywa chai ya yasimini ambayo hupatikana katika maduka ya mitishamba ya wachina. Kwa wale waliokwisha itumia wanasema chai hiyo inaufanya mwili ukae vizuri. Nami kwa uzoefu ninakushauri kunywa chai ya tangawizi ni chai bora. Kata vipande vidogo vya tangawizi na uweke kwenye kikombe cha maji moto ukinywa chai hiyo itakufanya uchangamke na kufanya ujisikie vizuri.
  4. Kumbuka matumizi bora ya muda yanakufanya kuwa makini zaidi katika yale uliyojipangia kuyafanya kwa siku husika na kufikia malengo yako bila wasiwasi.
  5. Katika kitabu au makala yeyote unayoisoma si lazima uyachukue yote na kuyatendea kazi kama vitabu vitakatifu. Angalia kulingana na mazingira yako ni yapi ya kukufaa yachukue hayo na kuyafanyia kazi. Na hapa unaweza kuona mfano katika makala yote au kitabu chote yumkini ukaona la kukufaa ni moja tu! Hiyo itakuwa ni sahihi. Lichukue hilo na kulifanyia kazi.
Kwa leo naishia hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram (+255 625 843 804)

Hakuna maoni: