- Harufu nzuri ndani ya chumba unachopumzika ina matokeo mazuri katika kumbukumbu na mwili wako. Mafuta yenye harufu ya chungwa na karafuu ni mazuri katika chumba unachopumzika. Kwa kufanya hivyo utahisi harufu nzuri ya amani na utulivu.
- Jijengee tabia ya kutembea japo dakika 30 usiku baada ya chakula na utembee maeneo yenye miti au maua ya asili, hili si tu ni mazoezi juu ya mwili wako bali hujenga afya yako pia. Ushahidi umeonesha kuwa wengi waliojizoesha kufanya hivyo hata katika uzee wao huonekana ni wenye nguvu kama vijana.
- Anza mazoezi ya viungo yatakayo inua uzito wako. Binadamu mwenye afya njema, ana uwezo mkubwa pia kiakili. Kadiri umri wako unavyoongezeka hupaswi kupunguza uwezo wa mwili ili akili yako iendelee kuwa bora pia. Ukiwa na umri wa miaka 75 bado kwa mwanaume unaweza kukimbia riadha, Aidha mwanamke wa umri wa miaka 80 unaweza kupanda milima. Na mzee wa miaka 90 bado unaweza kuishi maisha ya kiuzalishaji. Hii ina maana ikiwa umri wako ni miaka 19 au miaka 93 bado unaweza kuwa na nguvu na kuishi kwa matumaini na hamasa ya kimaisha.
- Usibishane na mtu unayemfanyia kazi kwani utapoteza zaidi ya mabishano yenyewe.
- Katika uvaaji kibiashara, suti nyeusi (blue bahari na nyeusi yenye kijivu) ina akisi uwezo, uchangamano na mamlaka. Je, umewahi kuona Raisi au Waziri mkuu akivalia vazi la suti ya rangi ya hudhurungi?
Kwa
leo naishia hapa na karibu tena,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au Whatsap/Telegram
(+255 625 843 804)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni