- Tawala vizuri sanaa ya usemaji mbele ya jamii yaani “the art of public speaking”. Wapo wasemaji wa asili wachache sana. Katika usemaji unaweza kuchukua falsafa za watu mbalimbali unaodhani ni maarufu na kuitumia katika kuwekea msisitizo ujumbe wako. Na ili matokeo yakushangaze hakikisha unaichukua picha ya msemaji huyo maarufu , unasimama kama yeye, unatabasamu kama yeye na kuzungumza kama yeye.
- Tafuta makala za kutia moyo toka kwa wasemaji maarufu kwa lengo la kujifunza tabia na kuwa na mafanikio endelevu. Na ufanye kama ni eneo la kuhudhuria mhadhara kila mwezi kwaajili ya kujiendeleza kama eneo muhimu la kujikumbusha. Semina ya masaa mawili , utajifunza mbinu thabiti na maarifa ambayo wengine walitumia miaka mingi katika kujifunza na kujisafisha. Usijione huna muda wa kupata mawazo mapya, unajiwekea akiba yako mwenyewe.
- Soma kitabu cha ajabu kiitwacho “Discovering Happiness” kama kilivyotolewa na “Dennis Wholey”. Ni hakika kitafungua upeo wa macho kwaajili yako katika kutafuta mahali sahihi pa afya na furaha yako.
- Katika kuongeza umakinifu wako, soma ukurasa japo mmoja katika kitabu ambacho hujawahi kipitia. Jaribu kukariri maneno ya kusimulia. Fanya hivyo kwa dakika tano tu kwa siku bila shaka utayafurahia matokeo yake baada ya miezi michache mbele ya jitihada zako.
- Jaribu kuingia katika riadha ya km.5 alafu baadaye km.10. Adrenalini inayotiririka kutokana na uzoefu wa mbio miongoni mwa watu 100 ambao wana kumbukumbu nzuri inaongezeka. Katika kusukuma kwa wastani bahasha iliyo katika uwezo wako, hiari yako itaongezeka kwa haraka. Kumbuka mwili wako utakuwa kama wewe mwenyewe unavyotaka uwe.
Kwa
leo naishia hapa,
\\ujasiriamaliafya
georgemtega@gmail.com au +255 625 843
804
Endelea
kufuatilia mambo haya kupitia www.ujasiriamaliafya.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni